24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

MZEE WA UPAKO: NITAJIZIKA MWENYEWE

Na FARAJA MASINDE-DAR ES SALAAM


mzee-wa-upako3MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu ‘’, ameibuka na kusema  alijiibua mwenyewe na atajizika mwenyewe.

Mzee wa Upako alitoa kauli hiyo mbele ya waumini wake wakati wa mahubiri ya  jana ndani ya kanisa lake,  Ubungo Kibangu, Dar es Salaam.

Vile vile katika mahubiri hayo, alikuwa akirusha vijembe kwa watu  wanaomnyooshea kidole kuwa katika siku za hivi  karibu alikutwa amelewa pombe akiwa mitaani.

Kiongozi huyo ambaye alianza kutoa mahubiri saa 6:5 hadi sa 7:15 mchana, alisema hakuna mtu aliyemuibua na kumpa upako akisisitiza kuwa alijiibua mwenyewe na atajizika mwenyewe.

“Hata wakisema, mimi sibabaishwi na magazeti, nilijiibua mwenyewe na nitajizika mwenyewe.

“Mbona hamkuwahi kusema Mzee wa Upako anaponya, sitafuti heshima bali inanitafuta yenyewe,” alisema.

Alisema anashangaa anavoona vyombo vya habari vikimchonganisha na Rais Dk. John Magufuli kwa lengo la kutaka kuwakosanisha, jambo ambalo alisema halitatokea.

Alisema hahitaji tenda yoyote kutoka serikalini, siyo mkuu wa wilaya wala mkoa, hivyo anamheshimu kama kiongozi na siyo Mungu.

“Kila wakiandika utasikia hivi karibuni sijui Rais Magufuli alitembelea kanisani hapo, mara alimpa barabara, sasa kwa taarifa tu ni kwamba amenipigia simu akanipa pole mtumishi wa bwana kwa mnavyonisakama.

“Pia amesema ataniongezea barabara kutoka hapa mpaka Makoka, maana sijui mlifikiri mkisema hivyo ndo ataninyang’anya hiyo barabara wakati ndiyo kwanza inazidi kuimarika.

“Sihitaji tenda yoyote serikalini wala safari za nje nazo zimefutwa… namuogopa Mungu tu na siyo mtu yeyote, hivyo usiyeheshimu madogo hata makubwa huwezi kuheshimu,” alisema.

Alisema ikifika mwakani mwezi kama huu, watu watajua uwezo wake  kwa sababu  angekuwa anafuga majini hakuna mtu ambaye angediriki kumwandika vibaya.

“Mwakani ndo mtajua mimi ni ‘Super Charge’.  Ninao uwezo wa kusema  ikifika Machi mwakani kila aliyeniandika vibaya afe halafu nawafungia mrlango.

“Hapa mmeshaingia choo cha kike, mimi ndiye zaidi ya Sheikh  Yahaya, nikiwarudia Iringa kwa muda wa siku saba tu sijui kama kuna atakayesalimika… kinyume na hivyo kama nitashindwa bora niache kuhubiri,” alisema.

Taarifa za Mzee wa Upako  kufanya vurugu, zilisambaa katika mitandao mbalimbali ya jamii huku video aliyorekodiwa eneo la tukio ikimuonyesha  akizungumza  maneno kama mtu aliyelewa pombe.

Chanzo cha tukio hilo kinadaiwa ni kulipiza kisasi kwa jirani zake hao wanaoishi katika nyumba namba KAW/MZN/1348, ambao alidai wamekuwa wakimkebehi kuwa hafai kuwa mchungaji kwa sababu ya ulevi.

Baada ya purukushani hizo, polisi kutoka katika Kituo cha Kawe walifika eneo hilo saa 3.00 asubuhi, wakamchukua   na kumpeleka kituoni.

Inadaiwa baada ya kufikishwa kituoni hapo, mchungaji huyo alipimwa kiwango cha ulevi na kukutwa kimefikia 131, ambacho kinaelezwa kuwa ni kikubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles