23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

MTOTO WA JICHO UGONJWA HATARI KWA WATOTO

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA


mtotoUGONJWA wa mtoto wa jicho kwa watoto umetajwa kuwa ugonjwa mkubwa kuliko magonjwa mengine ya macho.

Hayo yameelezwa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya macho, Dk. Frank Sandi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa ya mkoani hapa.

Alikuwa  akizungumza na waandishi wa habari katika kambi ya upimaji macho iliyoandaliwa na Taasisi ya Kiislamu ya Bilal (Bilal Muslim Mission) kwa kushirikiana na Mbunge wa   Dodoma, Anthony Mavunde.

Dk. Sandi alisema watoto wanaopokewa  wamekuwa wakionekana wana tatizo la ugonjwa wa mtoto wa jicho kuliko ugonjwa wowote wa macho.
Alisema kutokana na tatizo hilo ndiyo maana wataalamu hao wameamua kuweka kambi sababu pia ikitajwa kuwa ni vumbi linalopatikana Mkoani Dodoma.

“Kwa kawaida katika nchi ambazo hazina jua kwa kiasi kikubwa watu wanaopata ugonjwa huo ni kuanzia miaka 80 na kuendelea.

“Watu wajizoeshe kuvaa miwani ya kuzuia jua kwa kiasi kikubwa  kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa huu na vile vile wajenge tabia ya kupima afya ya macho mara kwa mara,” alisema.

Dk. Sandi alishauri wagonjwa wa shinikizo la damu (BP) na wale wa kisukari kuhakikisha wanapima afya zao za macho kwa sababu mara nyingi magonjwa hayo yanaenda sambamba.

Naye  Mavunde alisema ameamua kuwashawishi wataalamu wa macho kutokana na  ukubwa wa tatizo hilo na kwa kuwa Dodoma ni eneo la jangwa na hivyo kuwa na vumbi jingi.

Alisema katika kambi hiyo matibabu ya macho ikiwamo upasuaji, miwani na huduma za chakula, yatatolewa bure hadi hapo mgonjwa atakapopona na   kambi hiyo inahusisha watu wa wilaya zote.

“Nia yangu ni kuhakikisha natatua matatizo ya watu wa Dodoma.

“Hapa kwetu tatizo la macho ni kubwa hivyo ni lazima nikiwa kama mbunge niweze kutatua matatizo yao,” alisema.

Mratibu wa kambi hiyo, Ain Sharif alisema   watu 7,000 wameonwa katika kambi hiyo na wengine wakifanyiwa upasuaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles