25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mrema awashtaki Magereza kwa Waziri Mkuu

mremaNa MAULI MUYENJWA-DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Taifa wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema, amesema amepeleka malalamiko  kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kitendo cha Jeshi la Magereza kukwamisha mpango wa kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani.

Malalamiko hayo yamekuja, baada ya jeshi hilo kusitisha mpango wa kuwalipia faini ya Sh milioni 12.8 wafungwa 43 kwenye magereza mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma.

Faini zote za wafungwa hao, zingelipwa na Mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God ‘Mlima wa Moto’, Getrude Lwakatare.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mrema alisema  tayari fedha hizo zilishalipwa kwenye akaunti ya Magereza tangu Oktoba 21, mwaka huu, lakini wafungwa  hawajatolewa  hadi leo.

“Tunaamini kitendo hiki ni kinyume cha utawala wa sheria, ukiukwaji wa amri za mahakama ambazo zilieleza wazi endapo washtakiwa watalipa au kulipiwa faini waachiwe huru,” alisema Mrema.

Alisema awali kupitia Kanisa la Mchungaji Lwakatare, aliwalipia faini ya Sh milioni 25 wafungwa 78 kutoka magereza ya Keko, Segerea na Ukonga, Dar es Salaam.

“Hatujapewa sababu yoyote ya maandishi zinazosababisha wafungwa waliolipiwa faini wasiachiwe, tumepata taarifa kupitia vyombo vya habari kusitishwa kwa mpango huo na jeshi hilo,”  alisema Mrema.

Baada ya kusitishwa mpango huo, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Antonio Kilumbi, alinukuliwa na gazeti moja la kila siku (sio MTANZANIA) kuwa amesitisha mpango huo baada ya kupata maelekezo kutoka ngazi za juu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles