24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mishahara ya Vigogo wa Serikali yafyekwa

angellah-kairukiNa FARAJA MASINDE-DAR ES SALAAM

HATIMAYE agizo lililotolewa na Rais Dk. John Magufuli la ‘kufyeka’ mishahara ya vigogo wa Serikali, wakiwamo wa mashirika ya umma waliokuwa wakilipwa hadi Sh milioni 40 kwa mwezi, limeanza kutekelezwa.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam juzi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alisema tayari kazi ya ‘kufyeka’ mishahara hiyo imetekelezwa tangu mishahara ya Julai, mwaka huu.

Hatua hiyo, imekuja baada ya Rais Magufuli kuagiza kushushwa kwa viwango vya mishahara ya viongozi wa mashirika ya umma, ambao baadhi yao walikuwa wakilipwa Sh milioni 36 hadi 40 kwa mwezi.

“Tayari kazi ya kupunguza mishahara mikubwa ya watumishi wa umma imeshatekelezwa tangu malipo ya Julai, hakuna mtumishi yeyote wa umma anayelipwa zaidi ya Sh milioni 15,” alisema Waziri Kairuki.

Machi 30, mwaka huu akiwa wilayani Chato, Rais Magufuli alisema kuna watumishi wa umma ambao wanalipwa kiwango kikubwa cha mishahara na kujikuta wakiishi maisha kama malaika, hivyo ni lazima ishushwe  ili waishi kama shetani.

Hatua ya Rais Magufuli, kupitisha ‘panga’ na kuweka uwiano wa mishahara kwa watendaji wa taasisi hizo, inaelezwa kuwa itasaidia kuwapo uwajibikaji na usawa.

Rais Magufuli alisema kuwa ameunda timu ya wataalamu ambayo inafanya kazi ya kupunguza mishahara hiyo na kufikia Sh milioni 15 kwa mwezi ili asipatikane Mtanzania anayelipwa zaidi ya kiwango hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles