23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Chadema yaja na amsha amsha nchi nzima

chadema*Kufanya mikutano ya ndani siku 40

Na MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekuja na mkakati mpya wa mikutano ya ndani iliyopewa jina la amsha amsha itakayodumu kwa siku 40 nchi nzima.

Habari za uhakika ambazo MTANZANIA imezipata Dar es Salaam jana na kuthibitishwa na ofisa mmoja wa ngazi za juu wa chama hicho, zinasema viongozi wa Kamati Kuu na wabunge wote wa chama hicho watakutana mkoani Morogoro kuanzia kesho.

“Kweli kikao hiki kipo, viongozi wetu wa Kamati Kuu na wabunge wote wa chama tunakutana Morogoro kupeana majukumu ya chama chetu,” alisema ofisa huyo.

Alisema kikao hicho kitakachoongozwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kitakuwa na ajenda moja kubwa ya kupanga mikakati ya mikutano ya ndani kuimarisha chama hicho kuanzia ngazi ya kitongoji, kata, kijiji, wilaya na mkoa.

“Mbowe ataongoza kikao hiki kama mwenyekiti wetu, lengo letu kuwafikia wafuasi wetu kuanzia ngazi za chini, maana huko ndiko chama kilipo… tunafanya hivi kwa sababu mikutano hii imeruhusishwa na mamlaka husika,” alisema ofisa huyo.

Alisema katika kikao hicho, wanatarajia kuunda timu tatu ambazo zitazunguka kila jimbo la uchaguzi na kuweka mikakati yao.

“Tutaunda timu tatu ambazo zitapewa majukumu ya chama na kuzunguka nchi nzima, siwezi kukwambia nani atakuwa wapi, tusubiri kidogo itajulikana kuanzia kesho,” alisema ofisa huyo.

Hatua hii imekuja baada ya miezi kadhaa tangu chama hicho kutangaza kufanya maandamano na mikutano nchi nzima – Operesheni Ukuta ambayo ilisababisha Jeshi la Polisi kuipiga marufuku.

Operesheni hiyo iliyotarajiwa kufanyika Septemba mosi, mwaka huu, ambayo pamoja na mambo mengine ililenga kuishtaki Serikali ya Rais Dk. John Magufuli kwa umma kutokana na aina ya uongozi wake, iliibua mvutano mkali kati ya Chadema na Jeshi la Polisi.

Jeshi hilo lilitoa onyo kali kwa mtu yeyote ambaye angeandamana, huku kwa mara ya kwanza Watanzania wakishuhudia askari kila mkoa wakifanya mazoezi makali.

Baada ya mvutano huo, Mbowe alitangaza kuahirisha operesheni hiyo hadi Oktoba mosi, mwaka huu, kutoa nafasi kwa Rais Magufuli kufanya mazungumzo na viongozi wa dini kwa ajili ya upatanisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles