29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Al-Shabaab waua watu 12 Kenya

al-shabaabal-shabaabal-shabaab-2MANDELA, KENYA

WATU wenye silaha wanaoaminika kuwa wanamgambo wa al-Shabaab wameshambulia hoteli moja mjini Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya na kuua watu 12.

Msemaji wa Serikali ya Kenya, Eric Kiraithe amesema watu sita wameokolewa kutoka kwenye hoteli hiyo ya Bishaaro.

Wanamgambo walishambulia nyumba hiyo saa tisa na nusu usiku wakirusha mabomu kabla ya kuingia ndani na kuanza kuwafyatulia risasi waliokuwamo.

“Sehemu ya jumba iliporomoka na kuua watu 12. Watu sita wametolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo hilo wakiwa hai kufikia sasa,” ameandika Kiraithe kupitia mtandao wa Twitter.

Wataalamu wa mabomu wanafanya uchunguzi kubaini aina ya mabomu yaliyotumika kutekeleza shambulio hilo. Kundi la al-Shabaab limekiri kutekeleza shambulio hilo.

Mji wa Mandera umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa al-Shabaab, kundi linalopigana dhidi ya serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa (UN) katika taifa jirani la Somalia.

Wanamgambo hao wamekuwa wakishambulia zaidi watu ambao si wa asili ya Kisomali.

Hata hivyo, taarifa zilizotolewa baadaye na mratibu wa usalama eneo hilo, Mohamud Saleh zilidai waliotekeleza shambulio hilo si wanamgambo wa al-Shabab.

Saleh alisema kutokana na mpaka na Somalia kufungwa kuanzia usiku hadi alfajiri , hakuna namna kwa washambuliaji kuvuka mpaka huo.

Ameongeza kuwa uchunguz wa awali umeonesha shambulio hilo lilitekelezwa na magenge ya wahalifu walio na itikadi kali waliopo katika mji wa Mandera ambao walitumia mabomu manne kuilipua hoteli hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles