27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wafuasi wa Donald Trump wakamatwa Uganda

Donald TrumpKAMPALA, UGANDA

MAAFISA wa polisi nchini Uganda wamewakamata vijana wawili waliokuwa wakimfanyia kampeni mgombea urais kupitia Chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump katika ubalozi wa Marekani mjini Kampala.

Mtandao unaounga mkono Serikali Chimp Riports umesema vijana watano wa kundi la Young Democrats nchini humo walijaribu kuingia katika ubalozi wa Marekani.

Wafuasi hao wa Trump waliambiwa na maafisa wa polisi kwamba hawataruhusiwa kuingia ndani ya ubalozi kwa sababu walikuwa hawajapata ruhusa,kwa mujibu wa mtandao wa Chimp Report.

Trump katika Irani yake ya kampeni alisema kuwa atakabiliana na marais waliohudumu kwa muda mrefu kutoka Afrika akiwemo Rais Museveni.

Kwa sababu hiyo, ameondokea kujichotea wafuasi wengi nchini humo hasa wale waliochoshwa na utawala wa Museveni.

”Lazima tuonyesha umoja wetu na Trump”,Hakim Kizza ,mmoja wa wanachama wa kundi hilo alinukuliwa akisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles