29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Bulaya sasa kuanza kujitetea Oktoba 24

bulayaNa SHOMARI BINDA – MUSOMA
USHAHIDI wa Mbunge wa   Bunda mjini, Esther Bulaya, uliokuwa utolewe jana mahakamani katika kesi   ya kupinga matokeo ya ushindi wake   katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015   umeahirishwa hadi Oktoba 24.

Bulaya ataendelea na ushahidi wake tarehe hiyo baada ya Jaji anayesikiliza kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza inayokaa mjini Musoma, Noel Chocha, kuiahirisha kutokana na wakili anayemtetea mjibu maombi wa kwanza,Tundu Lissu,kufiwa na mama mkwe wake na Jaji kuwa safarini kikazi.

Wakati wa kuahirishwa kwa kesi hiyo Oktoba 13,Jaji Chocha alitupilia mbali  pingamizi 7 za aya 11 zilizokuwa kwenye kiapo cha Bulaya na kutaka zibaki aya nne pekee   kwenye kiapo chake cha ushahidi.

Pingamizi hiyo iliwekwa na  na wakili anayewatetea waleta maombi, Costantine Mutalemwa, waliofungua kesi hiyo kwa niaba ya Mbunge wa zamani wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Stephen Wasira.

Miongoni mwa mambo yaliyosababisha  Mutalemwa kuzipinga aya hizo ni kile alichoiambia Mahakama kuwa kuna mambo mapya ambayo yameelezwa kwenye kiapo katika aya ya 4 hadi ya 8 ambayo mwanzoni hayakuwapo kwenye maelezo ya awali ya mjibu maombi.

Wakili Mutalemwa aliiomba Mahakama kuziondoa aya ya pili, tatu, nne, tano ,sita, saba na nane na kubakiza aya nne pekee kati ya 11 zilizokuwa kwenye kiapo cha Bulaya.

Hali hiyo iliibua mvutano wa sheria mahakamani kati ya mawakili wa upande wa waleta maombi na wajibu maombi.

Wakili anayemtetea mjibu maombi wa kwanza, Tundu Lissu, baada ya kutoa vifungu vya sheria na kunukuu kesi mbalimbali  na Kanuni ya 23 ya Tangazo la Serikali namba 447 la mwaka 2010, aliiomba Mahakama kukataa pingamizi hizo kwa kuwa hazina msingi wowote.

Kwa upande wake wakili wa serikali, Angela Lushagamba, anayewatetea wajibu maombi wa pili na tatu ambao ni msimamizi wa uchaguzi na MMwanasheria wa serikali, alisema hakuwa na pingamizi lolote katika kiapo cha Bulaya.

Katika uamuzi wake,  Jaji Noel Chocha, baada ya kunukuu vifungu mbalimbali vya  sheria kwa saa mbili, alikubaliana na wakili Tundu Lissu, anayemtetea Bulaya  na kutupilia mbali pingamizi zote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles