24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Madaktari walia na uhaba wa dawa hospitalini

dawaNa Mwandishi Wetu -DODOMA

WAGANGA  wakuu wa mikoa na wilaya nchini wamemlilia Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakisema tatizo la ukosefu wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya afya  nchini limekuwa likisababisha malalamiko wa wananchi.

Mwenyekiti wa Waganga hao, Dk. Sudi Leonard amesema tatizo la ukosefu wa dawa na vifaa tiba limekuwa likizua manung’uniko kutoka kwa wananchi wanapokuwa wanahitahi huduma za tiba.

Alikuwa akizungumza katika mkutano wa mwaka wa wataalamu wa sekta ya afya kwa niaba ya waganga hao.

“Mheshimiwa makamu wa rais pamoja na mambo yote lakini tuna changamoto ya ukosefu wa dawa na vifaa tiba hali hii imekuwa ikisababisha malalamiko kwa wananchi.

“Mchakato wa upatikanaji wa dawa pia umekuwa ukichukua mchakato mrefu kutoka MSD mpaka kufika sehemu husika pia kuna hili kundi la watu maalumu na wao wanapokosa hulalamika,’’ alisema Dk. Leonard.

Alisema kwa sasa kuna upungufu wa watumishi wa sektra ya afya kwa asilimia 49 hali ambayo huwalazimu kufanya kazi katika mazingira magumu.

“Tunaiomba serikali itoe fursa ya ajira kwa sababu kwa sasa kuna zahanati 334 ambazo zinasimamiwa na wahudumu ambao siyo wataalamu wa afya,’’ alisema

Akifungua mkutano huo, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, alisema kutokana na hali hiyo ya ukosefu wa dawa Serikali imetenga Sh bilioni 70 kwa ajili kumaliza tatizo hilo.

“Tumetenga Sh bilioni 70 kwa ajili ya kumaliza tatizo la dawa nchini pia tumetenga   Sh bilioni 85 kwa ajili ya kupunguza deni MSD nia yetu ni kutaka huduma za afya ziwe zenye ubora,’’ alisema

Samia alisema Serikali ina mpango wa kujenga kiwanda cha dawa katika Mkoa ya Simiyu   kukabiliana na tatizo la dawa   nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles