25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Salumu Mwalimu, wenzake wapata dhamana

Salum MwalimuNa SAMWEL MWANGA

-BARIADI

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Simiyu imewapa dhamana viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akiwamo Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho   Zanzibar, Salum Mwalimu.

Hatua hiyo ilitokana na mahakama kutupa hoja za upande wa mawakili wa Serikali walioweka pingamizi la kutaka viongozi hao wasipewe dhamana kwa madai kwamba watahatarisha usalama wa taifa.

Hoja hizo za upande wa serikali ziliwasilishwa na  Mkaguzi wa Polisi, Mfelo Kusura kwa niaba ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Simiyu ambaye ilitaka washitakiwa wasipewe dhamana.

Hatua hiyo ilipingwa na mawakili wa upande wa utetezi ambao walikuwa wakiongozwa na wakili Godwin Simba na Martin Sabini   waliodai kuwa sheria hiyo ya Usalama wa Taifa haikutaja kifungu chochote na wala haiwezi kuzuia dhamana kwa washtakiwa.

Kutokana na mvutano huo, Hakimu John Nkwabi,  aliamua shauri hilo na kusema kuwa hoja zilizowasilishwa na upande wa Serikali si halali na kuzitupilia mbali.

Hakimu Nkwabi alisema  dhamana kwa washtakiwa hao iko wazi ila watakiwa kuwa na wadhamini wawili kila mmoja ambao watasaini bondi ya Sh milioni 20 pamoja na barua ya utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa.

Baada ya uamuzi huo washtakiwa wote walitimiza masharti ya dhamana   na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 4, mwaka huu.

Washtakiwa hao walikamatwa Agosti 23, mwaka huu katika Kijiji cha Dutwa wilayani Bariadi   wakidaiwa kupanga mikakati ya uchochezi kwa kupanga maandamano ya Septemba Mosi, mwaka huu yaliyojulikana kama Ukuta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles