28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenyekiti ACT asimamishwa

LIMBUNa Aziza Masoud, Dar es Salaam
HALMASHAURI Kuu ya Chama cha Alliance for Transparent (ACT), imemsimamisha uongozi Mwenyekiti wa Taifa wa muda wa chama hicho, Kadawi Limbu, na kumwondoa katika nafasi yake aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Leopold Mahona kwa makosa ya kinidhamu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa muda wa chama hicho, Samson Mwigamba, alisema hatua hiyo imekuja baada ya kamati maalumu ya kuchunguza masuala ya kinidhamu kujiridhisha kuwa kitendo alichofanya mwenyekiti huyo na wenzake kilienda kinyume na sheria na taratibu za chama.
“Baada ya mjadala wa kina na kujiridhisha kuhusu makosa yaliyofanywa na Limbu na wenzake, Halmashauri Kuu imeamua kumsimamisha katika nafasi yake kuanzia jana (juzi), sasa uongozi unafanya mawasiliano nae ili kumtaarifu kuhusu uamuzi huo,” alisema Mwigamba.
Alisema kati ya wajumbe 65 waliohudhuria katika kikao hicho, 57 ambao ni sawa na asilimi 85 walipiga kura ya kutokuwa na imani na mwenyekiti na katibu mkuu huyo huku wanachama sita walimkubali na kura moja iliharibika.
Mwigamba alisema makosa waliyofanya viongozi hao ni pamoja na kutangaza hatua haramu za kuwaondoa wanachama na kusababisha vurugu ndani ya chama.
Alisema viongozi hao pia walitumia nafasi zao na kuandika barua na kuipeleka kwa msajili wa vyama Aprili 27, mwaka jana, waliyokuwa wakiomba kuhairishwa kwa uchaguzi wa ndani ya chama hadi mwaka 2016 bila idhini ya wanachama.
Mwigamba alisema kwa mujibu wa sheria ya chama hicho ibara ya 17, kiongozi anaweza kusimamishwa na Kamati Kuu endapo atagundulika ameenda kinyume na sheria za chama.
Alisema Katiba ya chama pia inaruhusu kumsimamisha mwenyekiti na kutumika adhabu hiyo kwa muda usiopungua miezi sita.
Akizungumzia kuhusu uchaguzi wa ndani ya chama ambao ulikuwa moja ya ajenda za Halmashauri Kuu, Mwigamba alisema utaanza kuanzia Machi 17 kwa ngazi ya shina huku viongozi wa taifa watapatikana Machi 28.
Alisema kabla ya uchaguzi, kamati iliamua kuteua viongozi wa muda ambapo nafasi ya Katibu Mkuu wa Bara inashikwa na Mohamed Masaga huku Mwenyekiti wa Vijana Taifa atakuwa Hassan Abdallah Omari kutoka Zanzibar.
Aidha Halmashauri Kuu pia iliteua wajumbe wa bodi ya wadhamini wa chama wanaoongozwa na Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Kigoma, Gerald Mpango.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles