25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

NMB wajitoa malipo ya wastaafu hewa

2Na Jonas Mushi, Dar es Salaam

SIKU moja baada ya Rais Dk. John Magufuli kuweka wazi kuwapo Sh bilioni saba zilizolipwa kwa wastaafu hewa kupitia benki ya NMB,   benki hiyo imetoa ufafanuzi ikisema  huwa inafanya malipo kwa maelekezo ya mteja na si vinginevyo.

Juzi, Rais Magufuli akizungumza katika maadhimisho ya miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) alisema ukaguzi uliofanywa umebaini kuwapo k wastaafu hewa 2,800,  enki ya NMB ikiwa imelipa Sh bilioni saba kwa watu hao.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Mawasiliano wa Benki ya NMB, Joseline Kamuhanda, alisema benki hufanya malipo kwa mujibu wa maelekezo kutoka kwa mteja.

Kamuhanda alisema kama ilivyo kwa mteja yeyote mwenye akaunti anavyoweza kutoa maelekezo ya malipo yaende kwa mtu mwingine, ndivyo inavyokuwa katika malipo ya mafao na pensheni.

“Benki hatuwezi kumlipa mtu bila kupata ‘instructions’ (maelekezo) kutoka kwa mteja wetu na mtu yeyote mwenye akaunti ndiye anayesema mlipe fulani kiasi fulani na sisi kazi yetu inakua ni kulipa tu,” alisema Joseline.

Hata hivyo hakuweka wazi mteja aliyeelekeza malipo hayo yafanyike akidai  atakuwa amekiuka mkataba wa kutunza siri za mteja na kwamba serikali ndiyo inayoweza kuweka wazi zaidi.

Kauli ya SSRA

MTANZANIA ilimtafuta Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Uwezeshaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde, ambaye  alisema licha ya kutokuwa na taarifa rasmi kutoka kwenye mifuko hiyo  ukaguzi utaanza kulibaini  hilo na taarifa itatolewa rasmi.

Alisema malipo kwa wastaafu hufanywa kwa watu waliostaafu ambao taarifa zao hutolewa na mwajiri na mfuko ukisha kuhakiki ndiyo unalipa.

Kuhusu anayehusika kurudisha fedha zilizolipwa kwa makosa, alisema mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kiasi fulani itahusika kulipa kwa sababu ina wajibu wa kuhakikisha malipo yanakwenda kwa mtu sahihi.

“Mifuko ina kazi kuu tatu ambazo ni kuhakikisha malipo yanafanyika kwa mtu sahihi, kukusanya michango na kufanya uwekezaji, hivyo kama kuna watu ambao hawakustahili kulipwa lakini wamelipwa, watalazimika kurudisha fedha hizo,” alisema Sarah.

Hata hivyo alisema tatizo la wastaafu hewa linaanzia kwa mwajiri ambaye ndiye hupeleka taarifa za mtu aliyestaafu na anayestahili kulipwa pensheni pamoja na kodi.

Suala la   wastaafu hewa limeibuka baada ya ukaguzi maalumu wa watumishi hewa na tangu   Machi hadi Mei wamegundulika watumishi hewa 12, 246 na kuokolewa zaidi ya Sh bilioni 25.1 ambazo zingelipa mishahara ya watumishi hao hewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles