24.6 C
Dar es Salaam
Thursday, October 3, 2024

Contact us: [email protected]

Wilaya ya Serengeti yapiga marufuku mifugo kuzurura mtaani Mugumu

Na Malima Lubasha, Serengeti

Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara ,imepiga marufuku mifugo kuzurura katika mji wa Mugumu ikiwamo kuchunga ng’ombe, mbuzi na kondoo.

Kutokana na marufuku hiyo, msako wa kukamata mifugo umeanza baada ya kubainika wanaharibu mazingira kwa kula miti iliyopandwa

Tangazo la kuanza msako wa kukamata mifugo hiyo limetolewa Septemba 28, 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti,Kemirembe Lwota, akiwataka wananchi kuacha kuchunga mifungo ndani ya mji huo.

Imeelezwa kuwa watakaokaidi agizo hilo watalipa mfugaji sh 50,000 kwa ng’ombe mmoja, mbuzi na kondoo kila mmoja ni 20,000, hivyo wananchi wametakiwa kuheshimu sheria zilizopo kuzingatia maagizo ya serikali ya kuhifadhi uoto wa asili kwani hali hiyo inarudisha nyuma jitihada za serikali kulinda mazingira na tabia nchi.

Kwa mujibu wa maelekezo ya mkuu wa wilaya, wananchi au wafugaji wa ng’ombe,mbuzi ,kondoo wanatakiwa kufuga kisasa kwa kukata nyasi na kuwalisha ndani ya mabanda au kujenga mazizi vijijini kwani kuendelea kuchunga ndani ya mji inasababisha athari ya mazingira miti yote inayopandwa inaliwa na mifugo hiyo huku ikisambaza kinyesi chao ovyo.

Siku kumi zilizopita mkuu wa wilaya huyo, alikutana na wazee wa mamlaka ya mji mdogo mugumu kujadiliana maendeleo ya wilaya na nchi kwa jumla na kuwaonya juu ya kuachia mifugo.

“ Tunatakiwa kutunza mazingira kwa kupanda miti isiyopungua mitanonna kuendelea mara mvua inapoanza kunyesha kwani hivi sasa mji wa mugumu unapokea watalii wengi na mji wa kitalii hivyo usafi wa mazingira ni muhimu tuendelee kushirikiana na kutoa elimu juu ya kuhifadhi mazingira yetu na mji huu tusikubali muonekano na sifa ya Serengeti kimataifa ikapotea,” aliwaambia wazee hao.

Hata hivyo viongozi wa ngazi mbalimbali wilayani hapa wa vijiji,mtaa na vitongoji wametakiwa kuhakikisha wanahimiza wananchi kupanda miti, kulinda vyanzo vya maji na kuchukua hatua kwa wanaoharibu mazingira kwa kuchoma moto misitu katika maeneo yao ili kulinda Ikolojia ya Serengeti.

Lwota amesisitiza na kuwataka watu kuanza kuzitumia mvua zilizoanza kunyesha hivi sasa kwa kupanda miti ya aina mbalimbali ya kivuli ikiweamo ya matunda kwa ajili lishe na uchumi wa mtu mmoja mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles