24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 26, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mkuu ateta na Mwenyekiti wa Bodi ya CITIBANK

Na Mwandishi Maalum

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imekuwa inafanya kazi na benki ya Citibank ya Marekani kwa zaidi ya miaka 35 na imekuwa ikipokea ushauri wa mambo ya kifedha kupitia Benki Kuu ya Tanznaia (BoT).

Amesema hayo jana Septemba 24, 2024 alipokutana na Mwenyekiti wa Citibank, John Dugan, kwenye makao makuu ya benki hiyo, jijini New York, Marekani.

“Serikali ya Tanzania inaishukuru sana Benki ya Citibank kwa kuwa imeshiriki katika ujenzi wa uchumi ikiwemo na upatikanaji wa fedha za mikopo, kuishauri Serikali katik amasuala ya fedha na kufadhili miradi mikubwa inayoendelea kujengwa nchini,”

“Benki hii imekuwa ikikopesha makampuni yanayojenga reli yetu ya SGR na ili kuhakikisha wanachangia ujenzi wa uchumi wa Tanzania, na wao pia wamechukua lot moja ya ujenzi wa reli hiyo na kufadhili ujenzi wake. Hali kadhalika uendelezaji wa uwanja wa ndege wa Pemba,” amesema.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipeana mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Citibank ya Marekani, John Dugan, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo, jijini New York, Marekani. Septemba 24, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Ameeleza kuwa Tanzania ilipokabiliwa na uhaba wa mafuta ya kuendeshea mitambo na magari, hivyo benki hiyo ilitumika kuwasaidia wafanyabiashara kupata mafuta kwa bei nafuu.

Mbali na ushauri wa masuala ya kiuchumi, Waziri Mkuu amesema benki hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo ya Marekani, (U.S. International Development Finance Corporation) pia ilitoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo huku ikiwapatia fursa zaidi akina mama na wasichana wanaomiliki biashara zao binafsi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Citibank Marekani, Dugan amesema wataendelea kushirikiana na Serikali katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo kama walivyofanya katika miaka 40 iliyopita,

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles