26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

WHI kutekeleza mradi wa Nyumba 101 Mikocheni, Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Watumishi Housing Investments (WHI) inatarajia kuanza utekelezaji wa mradi wa nyumba 101 katika eneo la Mikocheni Regent Estate jijini Dar es Salaam. Ujenzi huo utaanza mwezi Agosti 2024, ambapo jengo la ghorofa 12 lenye nyumba 101 litajengwa. Kila mnunuzi atamilikishwa nyumba atakayoinunua, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma (Public Servant Housing Scheme) unaotekelezwa na WHI.

WHI tayari imejenga nyumba 1,003 katika mikoa 19 nchini Tanzania. Mradi huu mpya wa nyumba 101, ambao utekelezaji wake umekamilika kwa kusainiwa mkataba na Mkandarasi Shadong Hi-Speed Group leo, Julai 30, 2024, ni sehemu ya nyumba 218 zitakazojengwa katika mikoa ya Dodoma, Lindi, Mtwara, Singida, Pwani, na Ruvuma katika mwaka wa fedha 2024/2025.

Mradi huu wa nyumba 101 unakadiriwa kugharimu Sh bilioni 18.6 na utachukua miezi 18 kukamilika. Nyumba hizi zitauzwa kwa utaratibu maalum wa unafuu kwa watumishi wa umma.

Bei ya nyumba ya chumba kimoja itaanzia Sh milioni 99, huku bei ya nyumba ya vyumba vitatu vya kulala ikianzia Sh milioni 234. Bei hizi ni nafuu kwa asilimia 10 hadi 40 ikilinganishwa na nyumba za aina hii katika eneo la Mikocheni. Uuzaji wa nyumba hizo tayari umeanza, na mwitikio mkubwa unatarajiwa kutoka kwa walengwa.

Watumishi Housing Investments ni taasisi ya umma chini ya Ofisi ya Rais UTUMISHI yenye jukumu la uendelezaji wa milki na usimamizi wa uwekezaji kupitia uanzishaji na usimamizi wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja. WHI inasimamia mifuko miwili: Mfuko wa Nyumba na Mfuko wa Faida Fund.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles