Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku tano katika Mkoa wa Morogoro, itakayoanza Agosti 2 hadi 6, mwaka huu.
Ziara ya Dk. Samia inafanyika baada ya kutembelea mikoa kadhaa, ikiwemo Rukwa na Katavi, kama sehemu ya jitihada zake za kusikiliza kero za wananchi na kujionea maendeleo yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wake.
Ziara hiyo inafanyika wakati wananchi na wakazi wa Morogoro wakifurahia huduma ya usafiri wa reli ya SGR, ambayo imewezesha urahisi wa usafiri kati ya Dar es Salaam na Morogoro.
Wananchi mbalimbali mkoani Morogoro wanazungumzia kwa hisia kubwa ujio wa Rais Samia, wakitaja vipaumbele kadhaa vilivyosimamiwa na rais huyo, ikiwemo sekta za afya, elimu, na usafirishaji.