26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

NIT wapigia chapuo kozi za kimkakati

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimesema katika mwaka wa masomo wa 2024/2025 kinahamasisha vijana kusoma kozi za kimkakati kuiwezesha serikali kupata wataalam wazawa wa kutosha watakaosaidia katika ujenzi wa miradi ya kimkakati.

Akizungumza Julai 10,2024 kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Ofisa Uhusiano wa NIT, Juma Manday, amesema kozi hizo zinahusisha wataalam wa kujenga na kukarabati meli, wahandisi wa ndege, wataalam wa mafuta na gesi na wataalam wa kusimamia shughuli za bandari.

Amesema kutolewa kwa kozi hizo kutaiwezesha serikali kupunguza gharama hasa kwa sababu idadi ya watalaam wazawa itaongezeka.

“Mwaka huu tumekuja na kozi maalumu za kimkakati ambazo Serikali ya Awamu ya Sita imezipa kipaumbele katika mwaka wa masomo wa 2024/2025 utakaoanza Oktoba. Ni muhimu kwa miradi ya kimkakati ambayo serikali inaitekeleza.

“Tuna mradi wa kulifufua shirika la ndege, kujenga viwanja vya ndege na kuvipanua hivi vinahitaji watalaam, kwahiyo kozi za wahandisi wa kutengeneza ndege kwa sasa zinapata upendeleo wa mikopo kuanzia ngazi ya diploma,” amesema Manday.

Ofisa huyo ametoa wito kwa wahitimu wa kidato cha nne, sita na wengine kuchangamkia fursa ya kusoma kozi hizo ili kuiwezesha serikali kupata wataalam wa kutosha nchini.

“Natoa Wito kwa vijana waliomaliza kidato cha nne na wengine wachangamkie fursa iliyotolewa na serikali kwa kutoa kipaumbele kwenye kozi maalumu za kimkakati, waziombe ili waweze kuja kusoma kwenye chuo chetu na wanufaike na fursa ya kupata mkopo kughamia masomo yao,” amesema Manday.

Manday amesema katika maonesho hayo mbalimbali ya kutoa elimu ya shughuli mbalimbali wanazozifanya pia wamefanya udahili kwa wanafunzi wanaotaka kwenda kusoma katika chuo hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles