27.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi 250,000 elimu ya juu kukopeshwa Sh bilioni 787

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Wanafunzi 250,000 wa vyuo vya kati na elimu ya juu wanatarajia kunufaika na mikopo katika mwaka wa masomo 2024/2025 ambapo Sh bilioni 787 zimetengwa.

Idadi hiyo ya wanafunzi imeongezeka kutoka 224,056 wa mwaka 2023/2024 ambapo watakaonufaika ni wa shahada za awali, stashahada, stashahada ya umahiri katika mafunzo ya sheria kwa vitendo, shahada za umahiri na uzamivu na ruzuku za Samia.

Akizungumza leo Juni 6,2024 wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa uombaji mikopo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Dk. Bill Kiwia, amesema dirisha la kuomba mikopo kwa njia ya mtandao litakuwa wazi kwa siku 90 hadi Agosti 31,2024 na kusisitiza kuwa hawataongeza muda.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Dk. Bill Kiwia, akizungumza wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa uombaji mikopo kwa mwaka 2024/2025.

“Kwa uzoefu wetu siku 90 zinatosha kwa kuwa mwombaji akiwa amejiandaa na nyaraka zote muhimu inamchukua muda wa dakika 40 kukamilisha maombi yake kwa njia ya mtandao. Hivyo, tunasisitiza waombaji wa mikopo kuzingatia muda uliotolewa kwa kuwa hatutarajii kuongeza baada ya Agosti 31,” amesema Dk. Kiwia.

Amesema pia mwombaji atapaswa kuwa na akaunti ya benki na kwamba kwa waombaji wenye namba za nida watapaswa kuziweka wakati wa kuomba mkopo na kama mwombaji hana anaweza kuendelea na maombi bila namba hiyo.

Mkurugenzi huyo amesisitiza wanafunzi wanaoomba mkopo kusoma na kuzingatia maelekezo yaliyomo katika miongozo ya utoaji mikopo na ruzuku ambayo tayari imewekwa kwenye tovuti ya bodi hiyo ikiwa katika lugha za Kiswahili na Kiingereza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles