29.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Takukuru Ilala yabaini upotevu wa milioni 245 soko la Karume

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Ilala imebaini upotevu wa zaidi ya Sh milioni 245.1 katika Soko la Karume kwa kipindi cha Januari hadi Septemba 2023.

Upotevu wa mapato hayo ambayo ni ada za huduma ya usafi na ulinzi umechangiwa na kutokuwepo kwa taarifa za uhakika za idadi ya wafanyabiashara na kusababisha makusanyo pungufu kwa asilimia 47 ya makisio.

Akizungumza Januari 31,2024 wakati akitoa taarifa ya utendaji kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2023 Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Sosthenes Kibwengo, amesema wamefanya chambuzi za mifumo ya usimamizi wa ukusanyaji na matumizi ya ada za huduma za usafi na ulinzi katika soko la Karume na kubaini makusanyo pungufu.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Sosthenes Kibwengo, akimkabidhi cheti na fedha taslimu Asha Ally wa Shule ya Sekondari Zanaki baada ya kuibuka mshindi wa tatu katika shindano kuhusu nafasi ya vijana kuzuia rushwa.

“Tuliwaita viongozi wa soko na ngazi ya halmashauri, makisio wanayoweka kulingana na idadi ya wafanyabiashara hayaendani. Waweke mfumo wa kielektroniki kutambua idadi ya wafanyabiashara,” amesema Kibwengo.

Aidha amesema mkandarasi anayejenga vyoo vya umma jijini Dar es Salaam ametozwa faini ya Sh milioni 327.4 kwa kuchelewesha kazi kinyume na mkataba.

Takukuru ilifanya ukaguzi katika mradi huo wenye thamani ya Sh bilioni 3.27 unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) na kubaini kasoro kadhaa ikiwemo kuchelewa kukamilika hatua iliyosababisha mkandarasi kutozwa faini.

Kibwengo amesema pia wamepokea malalamiko 88 na kati ya hayo 54 yalihusu rushwa katika sekta ya elimu, ardhi, serikali za mitaa, afya na fedha.

Amesema mashauri mapya manane yakiwa na washtakiwa 24 yanayohusisha Sh bilioni 8.7 yalifunguliwa mahakamani ambapo 32 yanaendelea na mashauri matatu yenye washtakiwa watano yalihitimishwa kwa jamhuri kushinda.

Katika hatua nyingine taasisi hiyo imewazawadia vyeti na fedha taslimu wanafunzi wa sekondari ambao ni wanachama wa klabu za wapinga rushwa baada ya kuibuka washindi katika shindano kuhusu nafasi ya vijana kuzuia rushwa.

Wanafunzi hao na shule wanakotoka kwenye mabano ni Shedrack Raphael (Nguvu Mpya), Hellena Simon (Ilala) na Asha Ally (Zanaki).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles