25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 24, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Biteko asisitiza umuhimu wa ufuatiliaji na tathmini serikalini

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Dotto Biteko amesema kama Serikali haitafanya Tathmini ya shughuli zake haitakuwa na uwezo wa kujipima na vihatarishi vya utekelezaji wa mipango yake. 

Dk. Biteko ameyasema hayo mapema leo Septemba 12, jijini Arusha alipofungua Kongamano la Pili la Kitaifa la Ufuatilijai, Tathmini na Mafunzo ambapo amesema Serikali imegawanyika katika maeneo mengi kama vile Serikali Kuu na Serikali za Mitaa hivyo ufuatiliaji na tathmini ni eneo muhimu na linalopaswa kutiliwa mkazo.

Amesema kutokana na umuhimu huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan anasisistiza Serikali kuwa na Uratibu wa shughuli zake.

“Unaweza kukuta Serikali za Mitaa na Serikali kuu kila mtu anafanya jambo lake hakuna vinavyosomana, tujifanyie tathmini ili tusije kuwa watu wa kuduwaa kunini hili limetokeaje,” amesisitiza.

Dk. Biteko ameongeza kuwa asiyejifanyia tathmini atakuwa ni mtu wa hasara hivyo kujifanyia tathmini kunaifanya serikali kubaini matatizo mapema na kuweza kuyatafutia ufumbuzi kabla hayajaleta hasara.

Sambamba na hilo, Dk. Biteko amewataka maafisa masuhuli wote nchini kuviwezesha vitengo vya ufuatiliaji na tathmini katika wizara na taasisi zao kwa kuhakikisha kunakuwa na wataalamu wa kutosha, vitendea kazi na rasilimali fedha ili viweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulika na masuala ya (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama amesema wakati kongamano hili likifanyika kwa mara ya pili hapa nchini, Serikali imefanyia kazi kwa asilimia mia, utekelezwaji wa agizo la uanzishwaji wa Idara za Ufuatilijaia na Tathmini katika Wizara na Serikali.

Awali, akiongea wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dk. Jim Yonazi, alisema kwa kufuatilia mwendeno wa utekelezaji wa kujipima matokeo, Taasisi za Umma zinaweza kujihakikishia kuwa zipo katika njia sahihi za utekelezaji katika kufikia malengo yake, hivyo Ufuatiliaji na Tathmini ni njia nzuri ya kujifunza na kuwajibika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles