25.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 18, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mollel akutana na wazalishaji dawa za binadamu nchini kujadili changamoto

Na Esther Mnyika Mtanzania Digital

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel amekutana na wazalishaji dawa nchini na wanunuzi wa dawa nje ya nchi kutoa na kujadili changamoto mbalimbali ambazo zinazowakabili na jinsi gani ya kutatua changamoto hizo.

Hayo ameyasema Agosti 25 jijini Dar es Salaam alipokutana kwenye kikao na wadau mbalimbali Dk. Mollel amesema asilimia 84 ya vitu vya afya bado wanaagiza nje ya nchi na ndani asilimia 16.

“Kujadili changamoto gani? zinazowakabili walio jenga viwanda Tanzania na kuhakikisha tunaondoa vikwazo na tunaweka mazingira mazuri wawekezaji binafsi waweze kuzalisha na kupambana. katika soko,” amesema Dk. Mollel.

Amesema ni njia gani watafanya kuhamasisha watu wa nje kujenga viwanda ndani ya Tanzania na watapata faida kubwa na wananchi wanapata dawa kwa gharama nafuu.

Aidha, wadau wajenge viwanda vingi nchini wapunguze kununua dawa nje ya nchi.

Upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo amesema wadau kwa pamoja kujadili changamoto zinazowakabili katika dawa ni muhimu kuhakikisha dawa ni bora na hazina madhara yeyote.

“Kuhakikisha viwanda vya ndani kuzalisha dawa kupatikana kwa gharama nafuu na pia ni rahisi kudhibiti viwanda vya ndani vinavyoenda kinyume cha sheria,” amesema Fimbo.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Mavere Tukai amesema majukumu yao ni kuhakikisha na kuangalia namna ya upatikanaji wa dawa bora nchini.

“Dawa ni muhimu kwa wananchi na kuhakikisha zinapatikana kwa wakati. Mazingira bado ni changamoto kwa wadau wa kubwa tunaendelea kutengeneza fursa na mahusiano mazuri kwa wadau,” amesema Tukai.

Awali, Mwenyekiti wa Wazalishaji Dawa nchini, Churchill Katwaza amesema dawa ni muhimu kila nchi wanahitaji wazalishe dawa na vifaa tiba bora zinazokubalika kwa gharama nafuu.

Amesema changamoto ni nyingine zinazowakabili kwa sasa ikiwemo uhaba wa viwanda vya kuzalisha dawa viwanda vilivyopo hata 20 havifika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles