20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

COSTECH kuendelea kusimamia miradi ikiwemo Kigoda cha Utafiti SUA

Na Mwandishi wetu, Mtanzania Digital

TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imetaja vipaumbele vyake kwa mwaka 2023-2024 ikiwemo kuendelea kusimamia miradi mbalimbali.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Agosti 25,2023 na Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Dk. Amos Nungu wakati akieleza utekelezaji wa majukumu ya Tume hiyo na mwelekeo kwa mwaka wa fedha 2023-2024.

Mkurugenzi huyo ameitaja miradi hiyo ikiwemo Kigoda cha Utafiti katika SUA na NM-AIST ambao ni mradi wa miaka mitano, wenye thamani ya Sh bilioni 5.

“Pamoja na kushirikiana na Mabaraza ya Kikanda na Kimataifa kuhakikisha tunashiriki kutafuta fursa ambazo zitaendelea kuleta fedha za utafiti kupitia COSTECH au kuhamasisha Taasisi za ndani kuomba hizo fursa,” amesema Mkurugenzi huyo.

Pia, Kukamilisha zoezi la ufadhili wa pamoja miradi ya utafiti wa Mabaraza ya Utafiti duniani ikiwa ni njia mojawapo ya kuongeza kuonekana kwa watafiti na kuitangaza nchi katika nyanja ya utafiti.

Vilevile kukamilisha mchakato na kutoa fedha kwa maandiko mawili kwa kutoa mrejesho kwa walioshiriki lakini wakakosa, na kuwatembelea walioshinda.

Vilevile, kupitia mradi wa HEET, wanaboresha mifumo mbalimbali ili kuongeza ufanisi zaidi katika suala la uratibu wa umeme.

“Ikumbukwe kuwa mradi huu ni mahususi kwa Taasisi za Elimu ya Juu hivyo, inabidi tuwe tayari kuwahudumia baada ya kukamilisha mabadiliko wanayofanya kupitia mradi huo,”amesema Mkurugenzi huyo.

Pia,Kuwasaidia DTB kukamilisha karakana iliyopo SIDO Vingunguti ili kuzalisha mita kwa wingi na kwa wakati kukamilisha ufungaji wa mita hizo za maji kwa mikoa 15 iliyobaki.

“Kusimamia Kongano Bunifu mpya ikiwemo ya Mafia (nazi) na Kigoma (mawese) na kufanya kazi na kumbi za Bunifu na wadau wengine kuhakikisha mazingira wezeshi yanaimalika zaidi,” amesema Mkurugenzi huyo.

“Pia, katika kuratibu Utafiti na Ubunifu, COSTECH inaendelea kufanya kazi na wadau mbalimbali, ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa rasilimali fedha, sera na miongozo stahiki, mashirikiano, miundombinu, ili kuhakikisha mchango wa utafiti na ubunifu unaleta manufaa kwa taifa,”amesema Dk Nungu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles