Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital
KAMPUNI ya Azam Media imetambulisha tamthilia mbili za Kitanzania zinazofahamika kama ‘Mtaa wa Kazamoyo na Lolita’ ambazo zimebeba simulizi na kuleta mapinduzi ya tasnia ya tamthilia nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari, juzi jijini Dar es Salaam, Msimamizi Mkuu wa Chaneli ya Sinema Zetu, Sophia Mgaza amesema kuwa uzalishaji wa tamthia hizo mbili zimezingatia mahitaji ya soko kwani wametumia vifaa vya uzalishaji wa kisasa na ubora wa hali ya juu,” amesema Mgaza.
Aliongezea kwa kutoa rai jwa waandaaji wapya wanaongia na kazi zao za sanaa zinazoruka kwenye chaneli hiyo waweze kuhakikisha wanasimamia ubora wa kazi ili wasije kutoa sababu kwa watu wa pembeni kuwanyooshea vidole na kusema kuwa ilikuwa ni nguvu ya soda tu,” amesema Mgaza.
Pia amesema tamthilia hizo zinachukua nafasi ya Fungu langu itakayofikia tamati Julai 29, 2023 na Jeraha itakayofikia tamati tarehe 10 Agosti, 2023.