26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Chongolo kuunguruma Dar

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, anatarajia kuhutubia katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Dar es Salaam Julai 29,2023 katika viwanja vya Tanganyika Pakers Kawe.

Kufanyika kwa mkutano huo ni utekelezaji wa maazimio ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kilichokutana hivi karibuni jijini Dodoma ambacho pamoja na mambo mengine kiliazimia katibu mkuu kufanya mikutano katika mikoa mbalimbali ukiwemo Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abasi Mtemvu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 25,2023 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abasi Mtemvu, amesema katika mkutano huo wataeleza utekekezaji wa Ilani ya Uchaguzi uliofanyika Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi.

“Dhamira ya CCM ni kuendelea kuwaletea wananchi maendeleo, tunawaomba wananchi waje kwa wingi kwenye mkutano huu, tutaeleza utekelezaji wa Ilani na mambo mengi yanayoendelea nchini chini ya usimamizi wa Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema Mtemvu.

Chongolo anaendelea na ziara yake katika mikoa mbalimbali nchini ambapo tayari amefanya mikutano Mbeya, Mtwara, Lindi, Singida na Arusha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles