33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Mhagama akabidhi vitendea kazi kwa watendaji CCM

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Peramiho wamehimizwa kuendelea kushirikiana katika kusimamia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi na kuhakikisha Miradi ya maendeleo inafanikiwa na kutoa huduma sawa sawa kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama mbunge wa Peramiho wakati wa hafla fupi ya kukabidhi pikipiki tisa kwa watendaji wa kata CCM wa kata ya Peramiho, Maposeni, Ndogosi, Kilagano, Parangu, Kizuka, Litapwasi, Muhukuru, na Mpandangindo iliyofanyika Julai 8, 2023 mkoani Ruvuma.

“Vifaa hivi visaidie kukibeba chama kwanza, katika kusaidia kuongeza idadi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi katika maeneo yetu,” amesema Mhagama.

Ameongeza kuwa Jimbo la Peramiho ni miongoni mwa Majimbo yanayofanya vizuri, katika shughuli za serikali na shughuli za chama.

“Halmashauri ya Songea imepata hati safi mara mbili mfululizo, hiyo ni ishara kwamba uongozi wa chama na uongozi wa serikali wametambua wajibu wao,” alisema Waziri Mhagama.

Naye Mwenyekiti wa CCM Songea Vijijini ametoa rai kwa Watendaji wa Chama cha Mapinduzi kuendelea kuimarisha uwajibikaji na kumarisha mahusiano yao ya kiutendaji.

“Tuendelee kuwaimarisha na kuwasimamia waheshimiwa madiwani, kila mmoja kwenye eneo lake,” amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Songea, Menas Komba amesema watendaji wa chama wanapaswa kuhakikisha kura za chama zinapatikana kiutendaji kwa kuhakikisha mikutano inafanyika katika ngazi ya mabalozi na ngazi ya vitongoji.

Awali, Katibu Chama cha Mapinduzi Songea Vijijini, Juma Nambaila alisema moja ya eneo ambalo watalisimamia kikamilifu ni kuwapima makatibu wa kata kwa uwajibikaji wao wa shughuli za chama.

Akitoa shukrani Diwani wa kata ya Kizuka, Jackob Nditi amesema watatunza vitendea kazi na kuhakikisha wanashirikiana na watendaji wa chama kutekeleza maelekezo yanayotolewa na viongozi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama Mb) wa Peramiho akizungumza na Waheshimiwa Madiwani na Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Peramiho wakati wa Hafla fupi ya kukabidhi pikipiki.

P no 2 & 3

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama Mb) wa Peramiho akikabidhi pikipiki Watendaji wa Kata Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Peramiho

Pic no 4

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama wa Peramiho akiwa katika picha ya Pamoja na Watendaji kata wa Chama cha Mapinduzi wa Jimbo la Peramiho Wakati wa Hafla fupi   ya Kukabidhi Pikipiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles