22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali mbioni kukamilisha ujenzi wa Kidigital

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Serikali imesema iko katika hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa kidigitali ambao itawezesha kufikiwa kwa uchumi wa kidigitali duniani na kwamba kufikia hatua hiyo ni lazima sheria, sera na mikakati ifanane.

Akizungumza Julai 8, jijini Dar es Salaam wakati akizindua mtandao wa Intaneti ya wazi kwenye maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa sabasaba katika siku ya TEHAMA iliyoandaliwa na Tanzakwanza kwa kushirikiana na Tantrade, Waziri Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema kufikia ujenzi wa kidigitali ni lazima kuwa na miundombinu inayosaidia uchumi huo wa kidigitali ikiwa ni pamoja na kutengeneza vibao vya anuani za makazi.

“Lazima kuwe na sera ya wabunifu chipukizi katika eneo la kidigitali Kwani walioko chini wako vizuri kuwepo na sera itasaidia kuondoa utapeli, katika hili tunajipanga ili maonesho ya Sabasaba yajayo kuweka na vibao ili watu wanapofika katika viwanja hivi waelekezwe na vibao na kuongeza kuwa kama waziri anatamani kuliona hilo linafanikiwa,” amesema Waziri Nape.

Aidha, amesema katika uchumi wa kidigitali ipo haja ya minara ya mawasiliano kusambazwa nchini katika maeneo mbalimbali na kila wilaya iwe imeunganishwa na minara hiyo ya mawasiliano.

“Huko mbeleni tunataka wakuu wa wilaya wasitoke kwenye vituo vyao vya kazi kwenda mkoani Dodoma kwa ajili ya mikutano, wabakie walipo huko huko wakifanya kazi pia vituo vyote vya afya ziunganishwe katika huduma hii ya mawasiliano kidigitali,”amesema Waziri Nape.

Amesema mifumo hiyo inaweza kusaidia hata kurahisisha uendeshaji wa kesi mahakamani kwamba siyo lazima mshtakiwa kutoka mahabusu kwenda mahakamani bali taratibu zinaweza kuendelea, yakiwezekana hayo yote ni uchumi wa kidigitali ambao itasaidia kuondoa pia rushwa.

Amesema kazi kubwa kwa Serikali ni kuhakikisha mtandao uko salama uaminike na watu waweze kutumia ipasavyo, kuhusu maonesho aliitaka Tantrade kukutana na wadau kutoka wizara yake na kufanya tathmini kujua ni eneo gani la kuboresha kwani Serikali inataka watu wa kidigitali kuteka maonesho hayo.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade, Latifa Khamis amesema maonesho hayo imerahisisha biashara kwa njia ya digitali ambapo ukataji tiketi umefanikiwa kwa asilimia 95.

Amesema ugawaji wa sehemu za kufanyiwa biashara ulifanikiwa kwa asilimia 99 ambapo waombaji wengi walituma maombi ya vitambulisho jambo lililopunguza msongamano huku akiahidi kuwa wataendelea kuimarisha mifumo mbalimbali kidigitali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tanzakwanza Stragists, Tumaini Magila amesema kampuni hiyo imeandaa majukwaa nane ya kimkakati kuhakikisha jamii inapata uelewa wa kutosha.

Amesema katika uzinduzi wa mtandao, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfumo wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF), Albert Richard amasema yapo maeneo 17 katika viwanja hivyo na zaidi ya Sh milioni 200 zinatarajiwa kutumika katika uwekezaji huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles