NYOTA wa tenisi, Jamie Murray, atatakiwa kusubiri ili kuwa namba moja kwa ubora duniani baada ya kuambulia kipigo kwenye robo fainali kutoka kwa Mbrazil  Bruno Soares, kwenye michuano ya BNP Paribas Open, (Indian Wells Master).
Bila ushindi dhidi ya Feliciano Lopez na Marco Lopez, Murray alitarajia kuwa Mwingereza wa kwanza upande wa tenisi kuwa namba moja kwenye mchezo huo.
Tangu vyama vinavyosimamia viwango vya ubora katika tenisi (ATP na WTA) kutambulishwa mwaka 1970, haijawahi kutokea Mwingereza kuwa namba moja katika mchezo huo.
Hata hivyo, Murray alifanikiwa kufika hadi nafasi ya pili kwa ubora baada ya kushinda Grand Slam kwa upande wa wanaume kwa wachezaji wawili uliochezwa Januari jijini Melbourne, Australia.