24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Liverpool na Manchester United kitanzini

324EB12000000578-3497867-Manchester_United_s_Europa_League_clash_against_Liverpool_at_Old-a-1_1458289058669LONDON, England

TIMU za Manchester United na Liverpool zinatarajia kupigwa faini Mei 19 mwaka huu na Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), baada ya mashabiki wa timu hizo  kuonesha utovu wa nidhamu wakati timu zao zilipokutana kwenye mchezo wa marudiano hatua ya 16 bora, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Hatua hiyo ilitokana na mashabiki wa timu hizo kupigana baada ya mchezo kumalizika ambao uliifanya Liverpool kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-1.

Tukio hilo lilitokea baada ya mashabiki wa Manchester United waliokaa upande wa mashariki kuanza kushangilia kwa kuichoma kwa moto bendera ya Liverpool.

Tukio hilo lilisababisha mashabiki wa Manchester United na Liverpool kuingia kwenye ugomvi ambao ulikuja kuingiliwa na polisi na kuwakamata mashabiki watano.

UEFA inatarajia kutoa adhabu hiyo Mei 19, mwaka huu,  ambapo mashabiki wawili ni wa Liverpool na watatu kutoka Manchester United.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles