26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Murray atakiwa kusubiri kuwa namba moja duniani

Jamie-Murray-Wimbledon-Men's-DoublesLONDON, England

NYOTA wa tenisi, Jamie Murray, atatakiwa kusubiri ili kuwa namba moja kwa ubora duniani baada ya kuambulia kipigo kwenye robo fainali kutoka kwa Mbrazil  Bruno Soares, kwenye michuano ya BNP Paribas Open, (Indian Wells Master).

Bila ushindi dhidi ya Feliciano Lopez na Marco Lopez, Murray alitarajia kuwa Mwingereza wa kwanza upande wa tenisi kuwa namba moja kwenye mchezo huo.

Tangu vyama vinavyosimamia viwango vya ubora katika tenisi (ATP na WTA) kutambulishwa  mwaka 1970, haijawahi kutokea Mwingereza kuwa namba moja katika mchezo huo.

Hata hivyo, Murray alifanikiwa kufika hadi nafasi ya pili kwa ubora baada ya kushinda Grand Slam kwa upande wa wanaume kwa wachezaji wawili uliochezwa Januari jijini Melbourne, Australia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles