26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Khan atamba kumchapa Canelo

maxresdefaultLAS VEGAS, Marekani

BONDIA wa Uingereza, Amir Khan, ameibuka na kutamba kuwa yupo kwenye malengo ya kushinda mpambano wake dhidi ya Saul ‘Canelo’ Alvarez, utakaochezwa Las Vegas, Marekani.
Khan (29) ambaye anatarajia kupanda ulingoni Mei 7 mwaka huu katika uzito wa kati, alisema mazoezi yake yanaendelea vizuri kuelekea pambano hilo.
Khan na Alvarez tayari wapo kwenye kambi zao zilizopo Oakland na San Diego, wakijifua kabla ya pambano hilo litakalochezwa kwenye uwanja wa T-Mobile Arena, Las Vegas, Marekani
Nyota huyo alijigamba kufanya mazoezi kwa lengo la ushindi na kuongeza kuwa anatarajia ushindi wa kishindo dhidi ya mpinzani wake huyo.
Alvarez, ambaye ni mshindi wa mkanda wa WBC wa uzito wa kati baada ya kumdunda Miguel Cotton Novemba mwaka jana, anatarajia pia kutetea taji lake.
Nyota huyo alimkanya Khan na kumtahadharisha kwamba pambano hilo litakuwa gumu ingawa kila bondia anatarajia ushindi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles