26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Suarez atamba kuwa kwenye kiwango bora zaidi

Luis SuarezBARCELONA, Hispania

MSHAMBULIAJI wa timu ya Barcelona, Luiz Suarez, ametamba kuwa kwenye kiwango bora zaidi alipokuwa kwenye Ligi Kuu ya England.

Mchezaji huyo alidai kuwa uwezo wake wa ufungaji mabao msimu huu umeongezeka, huku akivutiwa zaidi na bao alilofunga kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal.

Mchezaji huyo alikamilisha mabao 43 kwenye michezo  yote msimu huu na kufanya jumla ya mabao tangu afike kwenye klabu hiyo iwe 68 katika michezo 84.

Mafanikio kwa mchezaji huyo yanaweza kumfanya kuwa miongoni mwa watakaowania tuzo ya uchezaji bora (Ballon d’Or) baada ya kuanza na mabao 17 ya Ligi Kuu Hispania.

Suarez alikuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo wa Liverpool akiwa pamoja na Raheem Sterling na Daniel Sturridge, ambapo kwa sasa akiwa Barcelona anashirikiana kwa karibu na Lionel Messi na Neymar.

Mchezaji wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher, alisema kuwa mchezaji huyo kiwango chake kimepanda tangu aondoke Liverpool mwaka 2014.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles