MKONGWE wa soka la Uholanzi, Marco van Basten, anaamini Memphis Depay si mchezaji wa kuisaidia Barcelona.
Depay alijiunga na Barca wakati wa usajili wa kiangazi akitokea Lyon na ameshafunga mabao matatu katika mechi sita alizocheza msimu huu.
Licha ya takwimu nzuri hizo, Van Basten aliyewahi kutamba na Ajax na AC Milan, amesema Depay anapenda kucheza mwenyewe na si kuisaidia timu, jambo ambalo ni hasara kwa Barca.
“Nashangaa kuona anacheza Barca,” amesema Van Basten aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018.