IMEBAINIKA kuwa beki aliyeondoka Arsenal, Hector Bellerin, alilazimika kupunguza mshahara wake ili tu akamilishe dili la kwenda kwa mkopo Real Betis.
Tangu kufunguliwa kwa usajili wa kiangazi uliofungwa juzi, Bellerin alikuwa akihusishwa na mlango wa kutokea Emirates, ikielezwa kuwa hakuwa kwenye mipango ya kocha Mikel Arteta.
Taarifa zinadai Bellerin alisamehe sehemu kubwa ya mshahara wake wa euro milioni 6.6 aliokuwa analipwa kwa mwaka pale Arsenal.
Hatua hiyo ya kukata mkwanja wake ilikuja baada ya Betis kutaka kuachana naye baada ya kuona wangeshindwa kumlipa.