28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

16 BORA KUWANUFAISHA LEICESTER CITY

LONDON, ENGLAND


leicester-city-soccer-teamWACHEZAJI wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini England, Leicester City, wanatarajia kupewa bonasi ya pauni 100,000 kwa kila mchezaji, baada ya timu hiyo kufanikiwa kuingia hatua ya 16 bora katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya.

Uongozi wa klabu hiyo ulitoa ahadi kwa wachezaji hao mapema kabla ya kuanza kwa michuano hiyo, ambapo waliambiwa endapo watafanikiwa kuingia 16 bora basi watapewa kila mmoja kitita hicho.

Kutokana na hali hiyo, jumla ya kitita cha pauni milioni 4.6 sawa na Euro milioni 5.5, klabu hiyo itapewa na Chama cha Soka barani Ulaya (UEFA), huku kila mshindi katika kundi akichukua kitita cha Euro milioni 1.5 sawa na pauni milioni 1.3.

Hata hivyo, uongozi wa klabu hiyo ya Leicester City umedai kuwa utaendelea kutoa zawadi kwa wachezaji hao endapo watafanikiwa kusonga mbele katika kila hatua kwenye michuano hiyo.

Kwa upande mwingine, kocha wa klabu hiyo ya Leicester City, Claudio Ranieri, amejivunia na timu hiyo kwa kuweza kuongoza katika msimamo wa kundi lao baada ya mchezo wa mwisho kushinda dhidi ya Club Brugge.

“Ni jambo ambalo si la kawaida kwetu kuweza kufanya makubwa kama haya ya kuongoza katika msimamo wa kundi letu, ni jambo la kushukuru kwa wote ambao walikuwa pamoja na sisi katika safari hii, nawashukuru wachezaji wangu, mwenyekiti wa klabu hii na wengine wote.

“Naweza kusema kwamba kazi yetu tumeikamilisha hadi kufikia hatua hii na tunatakiwa kugeukia kwenye michezo ya ligi kuu ili na huku tuweze kufanya makubwa kama tulivyofanya kwenye UEFA.

“Najua wachezaji wengi wamekuwa na furaha kubwa kwa timu yao kufika hapa, lakini sitaki waendelee kuifikiria hatua hiyo, nataka wafikiria juu ya kutetea ubingwa wa ligi kuu.

“Tupo katika wakati mgumu katika kutetea ubingwa, hivyo ni vizuri kupambana kwa kuwa tunaweza kushuka daraja tusipopambana kama ilivyo msimu uliopita, kama tunataka kupata kitu lazima tufanye hivyo sasa,” alisema Ranieri.

Kwa sasa klabu hiyo inashika nafasi ya 14 katika msimamo wa ligi, baada ya kucheza michezo 12 na kuwa na alama 12, huku Chelsea ikiongoza ligi ikiwa na alama 28 baada ya kucheza michezo 12.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles