29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

WILFRIED ZAHA ATAKA KURUDI AFRIKA

LONDON, ENGLAND


wilfried-zahaNYOTA wa klabu ya Crystal Palace, Wilfried Zaha, ameweka wazi nia ya kutaka kuitumikia timu ya taifa ya Ivory Coast, baada ya kuitumikia timu ya taifa ya England kwa michezo miwili.

Mchezaji huyo mzaliwa wa nchini Ivory Coast, aliwahi kuitumikia timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 21, lakini kwa sasa amedai kuwa anataka kubadili maamuzi na kujiunga na taifa lake la Avory Coast.

Zaha alikuwa na maamuzi ya kuamua kuitumikia England au Ivory Coast japokuwa tayari aliweza kucheza baadhi ya michezo ya timu ya taifa ya England.

Hata hivyo, mchezaji huyo amekosa nafasi ya kuitwa katika kikosi hicho, hivyo ameamua kufanya mpango wa kutaka kuitumikia timu ya Ivory Coast na si England tena.

Aliwahi kuitumikia England katika michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Sweden 2012 na dhidi ya Scotland mwaka 2013, lakini hakuwahi kupata nafasi ya kucheza katika mashindano yoyote akiwa na timu kubwa, hivyo anaweza kufanya maamuzi ya kurudi Ivory Coast.

Amedai kuwa hayo ni maamuzi sahihi kwake lakini anaweza kujiunga na timu hiyo mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani.

Sportsmail imethibitisha habari ya mchezaji huyo kutaka kurudi Afrika. Mwaka 2013, nyota wa timu ya Ivory Coast, Didier Drogba, aliwahi kusema kuwa atamshawishi mchezaji huyo kulitumikia taifa lake.

Msemaji wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), aliiambia Sportsmail kwamba jambo hilo linawezekana lakini bado halijafika kwenye ofisi zao na kama litafika basi litafanyiwa kazi.

Anachotakiwa kwa sasa mchezaji huyo ni kutuma maombi katika shirikisho hilo ili kuweza kufanyiwa maamuzi baada ya kujadiliwa.

Zaha mwenye umri wa miaka 24, alizaliwa nchini Ivory Coast, lakini familia yake ilihamia nchini England, huku mchezaji huyo akiwa na umri wa miaka minne, mchezaji huyo amewahi kukipiga katika klabu ya Manchester United na Cardiff.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles