27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

WENGER ATAKA WACHEZAJI KUTULIZA AKILI

LONDON, ENGLAND


wenger-arsene-arsenal_3412029BAADA ya klabu ya Arsenal kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Ufaransa, PSG, kocha wa klabu hiyo, Arsene Wenger, amewataka wachezaji wake kutuliza akili baada ya sare hiyo.

Wenger anaamini kuwa kuna baadhi ya wachezaji wamechanganyikiwa baada ya matokeo hayo, hivyo amewataka wachezaji wa aina hiyo kutuliza akili ili kufanya vizuri katika michuano ya Ligi Kuu nchini England.

Katika mchezo huo wa juzi ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Emirates, PSG walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 18 ambalo lilifungwa na mshambuliaji wao, Edinson Cavani, kutokana na kazi ambayo ilifanywa na Blaise Matuidi.

Arsenal walifanikiwa kusawazisha kwa mkwaju wa penalti ambao ulipigwa na Olivier Giroud, baada ya Aleix Sanchez kuchezewa vibaya ndani ya 18 katika dakika ya 45.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku wenyeji Arsenal wakitafuta bao la kuongoza na kufanikiwa kupata bao kabla ya PSG kusawazisha na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 2-2.

Kutokana na matokeo hayo, Arsenal wanashika nafasi ya pili katika kundi lao A, huku PSG wakishika nafasi ya kwanza wakitofautiana kwa mabao.

Wenger amedai kuwa walikuwa na lengo la kuongoza katika kundi lao, lakini wameshindwa kufanya hivyo ila si tatizo kwao kuwa kuwa bado wapo katika nafasi ya juu.

“Hatujapoteza mchezo, lakini tumepoteza nafasi ambayo tuliikusudia, hii yote inatokana na kukutana na timu bora, kwa sasa natakiwa kuwa makini katika kutoa matamshi yangu kwa kuwa watu wanaweza kuyasema yao,” alisema Wenger.

Wenger amewataka wachezaji wake kuhamishia nguvu zao kwenye michuano ya Ligi Kuu England ambayo inatarajia kuendelea wiki hii kabla ya kurudi kwenye klabu bingwa baada ya wiki moja.

“Hakuna haja ya ‘Kupanic’, wachezaji kwa sasa wanatakiwa kuangalia jinsi gani wanaweza kupambana kwa ajili ya timu yao kwenye michuano ya ligi kuu ili kuweza kujiweka sawa kwenye msimamo,” aliongeza.

Arsenal kwa sasa inashika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi nchini England, huku ikiwa na alama 25 baada ya kucheza michezo 12.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles