29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Spika Ndugai apigia chapuo ndege za ATCL

RAMADHAN HASSAN-DODOMA

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amewataka Watanzania kuthamini na kutoa kipaumbele katika kutumia usafiri wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ili kuinua uchumi wa nchi.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini hapa wakati wa ufunguzi wa ofisi za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL),  ambapo alisema kwa kufanya hivyo kutasaidia kuinua uchumi wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kuitangaza Tanzania kimataifa.

Alisema,huduma ya usafiri wa ndege nchini zimeboreshwa na kuwatoa hofu watanzania kuwa zile kero zilizokuwepo mwanzo hazitakuwepo.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Isaack Kamwelwe alisema wizara yake itaendelea kuboresha huduma za ATCL ili zizidi kuwa na ubora pamoja na kufika maeneo mengi nchini na nje ya nchi.

Alisema serikali watahakikisha  watanzania wote wananufaika na huduma za Shirikas hilo ikiwa ni pamoja na  kuongeza safari nyingi zaidi.

Waziri kamwelwe alisema Serikali kupitia wizara yake imedhamiria kuipa ATCL uwezo wa kushindana katika soko la kimataifa ikiwa na kununua ndege za kisasa.

“ATCL itaweza kuitangaza Tanzania katika masoko ya kimatifa kwa kununua ndege nzuri na za kisasa zitakazoweza kusafiri katika anga za kimataifa,”alisema.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi alisema  wataendelea kuboresha huduma za usafirishaji ili kuitanganza Tanzania nje ya mipaka.

Alisema mafanikio ya ATCL ni pamoja na kuona watanzania wanapata huduma nzuri pamoja na  kuboresha mifumo ya utoaji wa tiketi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles