20.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Wakulima wa korosho wanasema hawajalipwa kukwepa madeni – Waziri

Mathias Canal-Mtwara

WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga, ameagiza majina ya wakulima wote waliolipwa fedha za korosho, kubandikwa kwenye ofisi za vijiji kwa madai kuwa baadhi wanadai hajalipwa  kukwepa madeni waliyonayo vijijini.

Hasunga alisema hayo    mbele ya Kamati ya Bunge ya Mifugo na Maji kwenye kikao kazi kilichofanyika mkoani Mtwara.

 “Mimi nashangaa sana kila mkulima akiulizwa anasema hajalipwa, jambo hili siyo sawa nadhani wanafanya hivi kukwepa madeni wanayodaiana huko vijiji.

“Sasa naitaka timu ya wataalamu wa Operesheni Korosho kuhakikisha majina yote ya wakulima waliolipwa yanabandiikwa kwenye ofisi za vijiji.

 “Mpaka sasa tani 222,684 zimekusanywa na hadi Machi 14, Sh bilioni 596.9 zilikuwa zilishalipwa kwa wakulima kati ya Sh bilioni 723, lakini nashangaa wakulima wanasema hawajalipwa ,hili sio sawa,” alisema Hasunga

Alisema Serikali imejipanga hadi kufikia Machi 31, wakulima wote watakuwa wamelipwa fedha zao kwa vile uhakiki umekamilika kwa kiasi kikubwa.

Alisema   serikali ya awamu ya tano  inapaswa kuungwa mkono kwa uamuzi mgumu kwenye korosho kwa kuamua kuwalipa wakulima Sh 3,300 kwa kila kilo moja ya korosho.

Hasunga pia alidai kushangazwa na Mkoa wa Mtwara ambao unalima   karibu nusu ya korosho zote nchini lakini kuna idadi ndogo ya wafanyabiashara wanaofanya biashara ya korosho kinyume na sheria maarufu kama kangomba ikilinganishwa na mkoa wa Lindi ambao una idadi kubwa ya kangomba.

“Nashangaa sana Mkoa wa Mtwara una kangomba 10 lakini ndiyo wazalishaji wakubwa wa korosho huku Mkoa wa Lindi ambao unafuatia kwa uzalishaji wa korosho ukiwa na idadi kubwa ya kangomba ambao wapo zaidi ya 400,” alisema.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Dk .Christine Ishengoma, alimpongeza Hasunga kwa kuanzisha   usajili wa wakulima nchini.

“Nakupongeza   Waziri Hasunga kwa hili lakini hakikisha unalisimamia kwa weledi jambo hili liwe na matokeo chanya na wakulima waweze kutambulika kote nchini kwa sababu  kufanya hivyo serikali itakuwa na uwezo wa kuwahudumia kwa ufasaha,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,595FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles