25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

UVCCM Dar yazindua ‘Dar ya kijani’

ASHA BANI-DAR ES SALAAM

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dar es Salaam  umezindua kampeni ya ‘Dar es Salaam ya Kijani’ ikiwa na lengo la kurudisha mitaa na majimbo yaliyokwenda upinzani.

Kampeni hiyo inalenga kuweka mikakati kwa kuanzia ngazi za jumuiya zote za mkoa huo  kuanza kujipanga kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu  mwaka 2020.

Akizugumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo   Chuo Kikuu Kishirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) juzi, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, alisema   kampeni hiyo itachochea ustawi zaidi wa CCM katika Mkoa wa Dar es Salaam na kuzidi kukita mizizi katika ngazi zote kuanzia mkoa hadi majimbo, wilaya hadi kata, na matawi hadi mitaa.

“Leo tunazindua kampeni yetu ya “Dar es Salaam ya Kijani kuelekea serikali za mitaa 2019”, kampeni kabambe kwa ajili ya kuirejeshea CCM mitaa iliyopotea katika uchaguzi uliopita ambayo kwayo itatusaidia kupata ushindi mkubwa katika mkoa katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 wa udiwani, ubunge na urais.

“Sote tu-mashuhuda kwamba katika uchaguzi uliopita wa 2014 wa Serikali za Mitaa na ule Mkuu wa 2015 tulipoteza baadhi ya mitaa, kata na majimbo yaliyokuwa yakishikiliwa na CCM.

“Na sababu za kupoteza huko zinajulikana, sina haja ya kuzirejea sasa.

“Hivyo sisi vijana wa CCM tunatambua kuwa ndiyo damu na roho ya chama chetu, na kwamba tunao wajibu wa asili wa kusafisha njia katika kutimiza malengo ya uwepo wa vyama vya siasa kikatiba ya kushika dola,” alisema Kilakala.

Mwenyekiti huyo wa UVCCM, alisema   CCM inahitaji ushindi mkubwa kwa kuweka mikakati ya awali kwa kuwahusisha wanachama wa chama hicho wa ngazi zote.

“Kampeni yetu hii itashuka katika wilaya, kata na matawi yote katika Mkoa wetu   kuwa na ufahamu wa pamoja na kuhakikisha kila kijana wa UVCCM anawajibika ipasavyo kuhakikisha falsafa ya Dar es Salaam ya kijani yaani Dar es Salaam ya CCM inaenea kwa wanachama na wananchi ili ikifika wakati wa uchaguzi tuvune wapiga kura wa kutosha.

Mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa UVCCM,   Raymond Mwangwala, alisema ameridhishwa na kasi kubwa inayofanywa na vijana wa Dar es Salaam ya kuhakikisha chama kinapata heshima katika uchaguzi wote.

“Leo ninachokiona hapa, hii ndiyo UVCCM ninayoijua na sina shaka na uongozi wa mkoa kwa sababu  unafanya kazi kubwa na nzuri.

“Ninachoweza kusema kwenu ninawaomba sana vijana tukilinde chama na kuhakikisha tunapata ushindi katika uchaguzi wote.

“Na ikiwezekana si waachieni (upinzani) asimilia mbili tu ya mitaa na   ikibidi hata hakikisheni tunachukua asilimia yote 100. Vijana tushikamane  na tulinde heshima ya chama chetu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles