27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Zitto: Ngeleja anatapatapa

ngelejaFredy Azzah na Patricia Kimelemeta
SIKU moja baada ya Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), kumtumia Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe katika utetezi wake mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, kiongozi huyo amesema mtuhumiwa huyo anatapatapa.
Kauli hiyo ya Zitto imekuja siku moja baada ya kutoa maelezo yake mbele ya baraza kama njia ya kujinasua kwenye kashfa ya kunufaika na mgawo wa Sh milioni 40 kutoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Zitto alisema kutokana na kauli ya Ngeleja, anavitaka vyombo vinavyohusika vifanye uchunguzi mahususi dhidi ya tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake mara kwa mara, na ikiwa kuna Mtanzania yeyote ana nyaraka, yupo tayari kujibu mbele ya Baraza la Maadili.
Akihojiwa na Baraza la Maadili juzi, Ngeleja alisema Zitto amewahi kutuhumiwa kupewa Sh milioni 119 na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Shirika la Hifadhi ya Taifa (Tanapa).
Alisema licha ya tuhuma hizo kufikishwa bungeni, hatua zozote hazikuchukuliwa na kwamba wabunge kupewa fedha na mashirika ya umma na wafanyabiashara ni jambo la kawaida.
“Katika kujitetea mbele ya Baraza la Maadili kuhusu tuhuma dhidi yake za kugawiwa mgawo wa fedha kutoka akaunti ya Escrow, Ngeleja alisema ni kawaida wabunge kupewa misaada na wafanyabiashara na taasisi za umma.
“Katika maelezo yake alirudia tuhuma za kipuuzi dhidi yangu zilizokwishatolewa huko nyuma, kwamba nilipewa fedha na Kampuni ya PAP (Pan African Power) na nilipewa fedha na Shirika la NSSF,” alisema.
Alisema kutokana na kauli hiyo ya Ngeleja, amelazimika kurudia kutamka kwamba uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo ufanyike mara moja na watu wenye ushahidi wapeleke kwenye vyombo vya uchunguzi na kisha aitwe mbele ya Baraza la Maadili kujieleza.
“Nikiwa mbunge ambaye maisha yangu yote ya siasa nimeyatumia kupambana na ufisadi na kuchochea mabadiliko ili kujenga misingi madhubuti ya uwajibikaji na kuimarisha taasisi za Serikali, nipo tayari kwa uchunguzi mahususi dhidi yangu, dhidi ya tuhuma zilizotolewa na nyingine zozote ambazo Mtanzania yeyote anazo dhidi yangu.
“Tuhuma zote hizo nimewahi kuzitolea ufafanuzi na kukanusha kwani hazina msingi wowote na zilikuwa siasa za majitaka. Hata hivyo bado zimekuwa zikijirudia rudia kwa malengo maalumu wanayoyajua wanaotoa tuhuma hizo,” alisema Zitto.
Alisema watuhumiwa wa ufisadi wa Escrow hawajazoea kuona taasisi za maadili zikifanya kazi kwa namna ilivyo sasa, hivyo wanajaribu na watajaribu kubwabwaja na kuhangaika ikiwamo kutaka kila mtu aonekane ni mtuhumiwa kama wao,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles