26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Zitto, Mwigulu wang’ara urais 2015

Zitto-KabweNa Asifiwe George, Dar es Salaam
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) ameng’ara katika mbio za urais mwaka 2015 akipata asilimia 18 tofauti na wagombea wengine wanaotajwa kugombea nafasi hiyo kupitia muungano wa vyama vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), utafiti umebaini.
Takwimu hizo zilitolewa na Asasi ya Utafiti wa Elimu Tanzania ( TEDRO) kwa lengo la kutathmini ushiriki wa vijana katika siasa kama wagombea na namna ambavyo vijana wanavyopokewa katika jamii.
Akitoa ripoti hiyo Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa TEDRO, Jacob Kateri, alisema takwimu hizo zinaonesha kuwa Zitto ni kijana anayepewa nafasi kubwa endapo atapeperusha bendera ya Ukawa.
Katika utafiti huo Zitto anafuatiwa na Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia kwa asilimia 16, Tundu Lissu (14), John Mnyika (7), David Kafulila (6), Julius Mtatiro (4), Moses Machali (4) na Joshua Nasari (2).
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu (bara) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwigulu Nchemba alionekana kuwapiku wenzake kupitia chama hicho kwa asilimia 38, akifuatiwa na Dk. Emmanuel Nchimbi (26), Januari Makamba (24), William Ngeleja (11), Lazaro Nyalandu (100, Hamis Kigwangala (7), Deo Filikunjombe (5) na Esther Bulaya (2).
Kateri alisema utafiti huo ulilenga kuchambua malengo mahususi manne ambayo ni ushiriki wa vijana katika siasa kama wagombea, mchango wa wanasiasa vijana katika kufuata misingi ya utawala bora, uwajibikaji na utelezaji wa ahadi za wagombea.
Kateri alisema utafiti huo uliweka sababu mbalimbali ambazo ni kichocheo kwa vijana kuingia katika siasa zikiwemo uzalendo asilimia 67 kimbilio baada ya kukosa ajira (57), uwezo mdogo wa watangulizi wao katika nafasi husika (60), mafanikio ya wanasiasa vijana walio mahiri (72), vyama vya siasa kuwapa nafasi vijana katika vyama vyao (59) na kukubalika kwa vijana sababu ni vijana 63.
“Utafiti huu umeandaliwa na kufanyika Tanzania Bara na ulifanyika katika wilaya 18 na utafikia kila kanda ukiwa umehusisha wilaya moja hadi tatu huku kila wilaya vimehojiwa vijiji vitatu na watu 15.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles