27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Ngassa aipa raha Yanga

pg32JENIFFER ULLEMBO NA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM

TIMU ya Yanga jana ilifanikiwa kurejea kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kuichapa Mtibwa Sugar mabao 2-0 mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Yanga imewashusha waliokuwa vinara Azam wenye pointi 22 baada ya kufikisha jumla ya pointi 25, lakini wanalambalamba hao wana mchezo mmoja mkononi.Winga wa Yanga, Mrisho Ngassa ndiye aliyeibuka shujaa kwa timu yake baada ya kuifungia mabao hayo yote, akiwa ameingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mliberia, Kpah Sherman.
Kipigo hicho kimeifanya Yanga kulipa kisasi cha kufungwa na Mtibwa kwa idadi hiyo ya mabao, mchezo uliofanyika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, wakati huo
Yanga ilikuwa ikinolewa na Mbrazil, Marcio Maximo.Yanga ilianza kwa kasi
pambano hilo iliyopelekea dakika ya tatu mshambuliaji wake, Amissi Tambwe kukosa bao la wazi baada ya kupigwa kichwa kilichotoka nje ya lango la Mtibwa wakati akiunganisha krosi ya Andrey Coutinho.Winga wa Yanga, Simon Msuva
itabidi ajilaumu mwenyewe dakika ya 31 baada ya kushindwa kumalizia vema shuti lililotemwa na kipa wa Mtibwa, Said Mohamed, kufuatia shuti kali alilopiga Tambwe akiwa nje kidogo ya eneo la 18 Dakika chache baadaye Kocha wa Yanga, Hans van Pluijm, alifanya mabadiliko kwa kumtoa beki wake, Edward Charles aliyeumia na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Abdul. Lakini hadi dakika 45 zinamalizika timu hizo zilitoka suluhu. Kuingia kwa Ngassa dakika ya 50 na kutoka Sherman aliyeonekana kupwaya kutokana na kukaa na mipira sana kila wakati bila sababu, kuliimarisha eneo la ushambuliaji la Yanga ambao walilisakama lango la Mtibwa kama nyuki.
Ngassa aliyekuwa hana furaha kutokana na deni analodaiwa benki, alitumia dakika tano baada ya kuingia na kuifungia timu yake bao la uongozi dakika ya 55, aliyeunganisha krosi ya Msuva iliyomshinda kipa wa Mtibwa Sugar.
Yanga ilizidi kulisakama lango la wapinzani wao na alikuwa Ngassa tena aliyezidisha machungu kwa kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime, baada ya kumlamba chenga kipa wa timu hiyo na kufunga bao safi dakika ya 62 na kuihakikishia pointi tatu muhimu timu yake.
Bao hilo lilizidi kuwanyong’onyeza Mtibwa ambao walionekana kuchoka huku Yanga ikizidi kulisakama lango lao, lakini hadi dakika 90 zinamalizika, wanajangwani hao waliondoka na ushindi huo. Wakati huo huo Yanga inatarajia kuingia kambini leo jioni kwenye Hoteli ya Tansoma kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya timu ya BDF XI ya Botswana utaofanyika Jumamosi hii jijini Dar es Salaam.Yanga itakuwa ikifanya mazoezi
yake kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hadi itakapovaana na Wabotswana hao wanaoshika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu Botswana kwa pointi 37.Majimaji yarejea Ligi KuuWakati huo huo, timu ya Majimaji ‘Wanalizombe’ ya Ruvuma imefanikiwa kupanda
Ligi Kuu baada ya kuifunga Mlale JKT mabao 2-1 mchezo uliofanyika Uwanja wa Majimaji ya Songea.Majimaji imepanda baada ya kufikisha jumla ya pointi 42, mabao yake yalifungwa na mshambuliaji mkongwe Kudra Omary na Bitram Nchimbi.
Timu hiyo imeungana na African Sports ya Tanga iliyotangulia kupanda Ligi Kuu zote zikiwa ni timu za Kundi A za Ligi daraja la Kwanza na sasa Majimaji imebakiza mchezo mmoja dhidi ya Kimondo FC ya Mbeya.Mpinzani wake aliyekuwa akiikaribia, timu ya Lipuli ya Iringa yenyewe imeambulia sare ya bao 1-1 dhidi Polisi ya Dar es Salaam, huku mchezo wa Friends Rangers dhidi ya Kimondo ukiahirishwa baada ya mvua kubwa kunyesha.
Mchezo huo uliahirishwa dakika ya 48 wakati timu hizo zikiwa sare ya bao 1-1, hivyo hata Friends Rangers ikishinda mechi zake mbili za mwisho itafikisha pointi 41 ikiwa ni pungufu ya pointi moja dhidi ya majimaji

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles