26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Zitto: Benki Standard ichunguzwe kwa rushwa

Zitto_Kabwe_2011Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MBUNGE wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, amesema Benki ya Standard inapaswa kuchunguzwa kwa rushwa kuhusu suala la hati fungani ya Dola za Marekani milioni 600.

Amesema kwa sasa deni la Taifa limepanda na kufikia dola bilioni 15  sawa na Sh trilioni 30, ambapo kutokana na ukubwa wa deni hilo, Tanzania hulipa huduma ya deni la Taifa takribani Sh trilioni 2.2 kila mwaka.

Alisema licha ya hali hiyo bajeti ya kuhudumia deni la Taifa ni kubwa zaidi kuliko bajeti ya wizara yoyote nchini.

Alisema kutokana na suala hilo katika madeni hayo yapo ambayo yamepatikana kwa rushwa na mengine yamechukuliwa kwa matumizi ya anasa.

“Kitaalamu madeni haya yanaitwa ‘Odious debts’. Moja ya Deni la hovyo ni la dola za Marekani milioni 600 ambalo Tanzania ilikopa kutoka Benki ya Standard ya Uingereza kupitia hati fungani.

“Taasisi ya SFO ya Uingereza inayoshughulika na rushwa kubwa imeonyesha kuwa mkopo huu ulipatikana kwa rushwa. Taasisi ya Corruption Watch ya Uingereza imeonyesha kuwa Tanzania imepata hasara ya takribani dola milioni 80 sawa na bilioni 160 kwa kuchukua mkopo huu.

“… hata hivyo uchunguzi wa SFO haukuhusisha maofisa wa juu wa Standard Benki makao makuu na hivyo kufunika kombe mwanaharamu apite.

“Iwapo uchunguzi ungegundua kuwa Standard Benki walihusika moja kwa moja na hongo hii, Tanzania ingefutiwa deni lote na kuokoa fedha nyingi sana ambazo zingewekezwa kwenye sekta za elimu, afya na maji,” alisema Zitto.

Mbunge huyo wa Kigoma Mjini, alisema wanaitaka Benki ya Standard ya Uingereza ichunguzwe upya na SFO kuhusu tuhuma za rushwa ili kupata biashara Tanzania ya hati fungani pamoja na kujua ukweli wa kile alichodai ufisadi huo.

Kutokana na hali hiyo alisema wameandaa maombi kwa kuitaka FSO ya Uingereza ifungue upya uchunguzi kwa kuzingatia ushahidi mpya kuwa mabosi wa Benki ya Standard ya Uingereza walihusika na mipango ya kutoa hongo ili kupata biashara Tanzania.

Alisema ikibainika mabosi hao walishiriki maana yake Tanzania itafutiwa deni lote kwa sababu benki hiyo itawajibika kurudisha fedha za watu kwani Hati fungani itaonekana ni batili.

Zitto hivi sasa Tanzania inaanza kulipa deni hilo kuanzia Aprili, mwaka huu na kama wasipozuia tunazuia kwa maombi haya kwa FSO.

Alisemas iwapo deni hilo litalipwa juhudi za Rais Dk. John Magufuli, kupata mapato zitaathiriwa na sekta nyeti kama elimu, afya na maji zitakosa bajeti ya kutosha.

Alisema kutokana na hali hiyo aliwaomba Watanzania kote duniani kuitaka SFO ifungue uchunguzi kwa kuzingatia ushahidi mpya dhidi ya Benki ya Standard ambayo sasa inaitwa ICBC plc

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles