22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Zitto atwaa tuzo utetezi haki hifadhi ya jamii

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), ameibuka mwanasiasa wa kwanza barani Afrika kwa kutwaa Tuzo ya Mtetezi wa Haki ya Hifadhi ya Jamii.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mwishoni mwa wiki na Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya Nchi za Afrika Mashariki na Kati (ECASSA), ilieleza mbunge huyo aliibuka mshindi.

Zitto anatarajiwa kukabidhiwa tuzo yake hiyo katika sherehe rasmi iliyopangwa kufanyika Oktoba 30 na 31 mwaka huu katika mji wa Livingstone nchini Zambia.

“Tuzo hii imetolewa kwako kwa kuzingatia mchango wako mkubwa unaoutoa kuhakikisha sehemu kubwa ya Watanzania ambao walikuwa hawanufaiki na mifuko hii wanafaidika nayo.

“ECASSA, mahususi kabisa, imevutiwa sana na jitihada zako za kuhakikisha kwamba wasanii wananufaika na mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na wakulima kupitia chama chao cha ushirika cha Rumako kilichopo Kigoma Vijijini,” ilisema sehemu ya barua ya umoja huo kwa Zitto.

Akizungumzia tuzo hiyo, Zitto alisema: “Nimeipokea tuzo hii kwa unyenyekevu mkubwa. Naamini kuwa siku za usoni haki ya hifadhi ya jamii kwa wananchi itakuwa ni haki ya kikatiba.

“Nchi masikini zinapaswa kuongeza uwekaji akiba ili ziweze kuendelea kwa kasi. Bila akiba uwekezaji unakuwa mdogo na hatimaye uchumi haukui,” alisema.

Azimio la kutolewa kwa tuzo hiyo lilitokana na Mkutano Mkuu wa Sita wa ECASSA uliofanyika jijini Kampala, Uganda miaka miwili iliyopita.

ECASSA ni umoja unaounganisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii takribani 20 katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Zambia.

- Advertisement -

Related Articles

2 COMMENTS

  1. Hongera sana Mheshimiwa Zitto.Tuzo hiyo bila shaka inakupambanua kuwa pamoja na ukweli ni kwamba wewe ni Mwanasiasa, sio miongoni mwa wale WACHUMIAMATUMBO kwamba kwako siasa sio tu chombo cha kukujenga wewe binafsi na walio karibu nawe, bali unajali maslahi na ustawi wa Jamii inayokuzunguka. Kwa upande huo wa Hifadhi ya Jamii napenda kuungana na Wastaafu na Watumishi pamoja na Wanachama wengine wa Mifuko ya Jamii utupie jicho uamuzi wa Serikali kupitia upya mfumo wa ukokotoaji wa mafao unaokusudiwa kuanza kutumika ambao umeanza kulalamikiwa kwamba utawapunja Wanachama wa Mifuko husika. Aidha, upo umuhimu wa kuangalia hata utaratibu wa ulipaji na viwango vya sasa vya mafao, kwani hauendani na kupanda kwa gharama za maisha ikilinganishwa na faida inayotengenezwa na Mifuko ya Jamii katika uwekezaji wa fedha za Wanachama. Tunasikia serikali ni mdaiwa mkuu wa mifuko hii. Je sheria ya udhibiti wa mifuko hii inaruhusuje hali hii ya serikali kujichotea fedha inavyotaka huku Wanachama wenye fedha hizo tukiteketea?

  2. Mheshimiwa Zitto nakupongeza sana tena sana pamoja na wote wanaokuunga mkono katika majanga haya ya ufisadi Mungu wetu azidi kuwaweka katika ulinzi wake msipatwe na mabaya. Watanzania wengi tunajiuliza je! shutuma hizi ambazo zimefukunuliwa na baadhi kuzituhumu si za kweli na kisha kwa upekuzi na uchunguzi mambo yakajidhihirisha ni kweli kama zisingetolewa kujulikana tokea EPA, RICHMOND, na sasa IPTL sisi watanzania tungekuwa tumetesekaje? wachache hao ndio wangezidi kuneemeka. Watanzania tuwe pamoja na vijana wetu hawa wanaojiweka kifua mbele kutetea haki za vizazi vijavyo. Tusijidanganye na kushiba kwa siku ya leo lakini kesho hujui utakula nini. Tupo kabisa kuwaombea na kuwaweka katika sala ili taifa hili liondokana na balaa hili la uchoyo uliyokidhiri. Je wewe uliyechukua ama uliye na mabilioni katika account zako ziwe hapa Tanzania ama huko Ulaya saa hii Mungu wako aliyekuumba anaitaka roho yako zote hizo zitaleta manufaa kwako huku uendako? ama ni kilio na kusaga meno? Tusaidieni nyie ambao mnaotuhumiwa kuchota hata hayo mamilioni kuleta maendeleo katika nchi ambayo yatawanufaisha watanzania wote na sio koo zenu tu. Tumwogope Mungu na tunukuu maneno ya Baba yetu Mwl Nyerere aliyosema kuwa kiongozi lazima awe na hofu ya Mungu ili kutenda yale yalio mema. Hongereni na ingekuwa ni watanzania kuwa ni kuwatunza kwa zawadi hata mahali pa kuziweka pasingetosha lakini zawadi toka kwa Watanzania wengi ni SALA KWENU.Fichueni yote ili tuzidi kuanza na uadilifu 2015 udumu katika nchi kwa kuonyesha adhabu kali kwa wote watakaohusika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles