32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Zitto ashauri kuanzishwe mfuko wa hifadhi kwa wakulima wa korosho

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam


Chama cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuanzisha mfuko wa hifadhi ya wakulima wa korosho ili kuwekwe fedha ambazo lengo lake ni kusaidia kuendelea na uzalishaji pindi bei ya zao hilo ikishuka katika soko la dunia.

Kauli hiyo imetolewa leo na kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Makao makuu ya ACT- jijini Dar leo Jumapili Oktoba 28, ambapo amesema wakulima wanaathirika bei zinaposhuka kwasababu wanatumia gharama kubwa katika uzalishaji na wanapata fedha kidogo zaidi ya walizowekeza na hali hii inakatisha tamaa.

Amesema kwa wiki mbili sasa kumekuwepo na mjadala juu ya bei ya korosho ambapo bei elekezi iliyotolewa na serikali kwa mwaka huu Sh. 1,550 kwa kigezo kuwa mkulima ananunua dawa ya Sulphur kwa Sh. 32,000 kwa mfuko, hivyo ikikikadiriwa kuwa gharama za uzalishaji kwa kilo moja ya korosho ni Sh. 1,350 kwa bei hiyo atapata faida ya Sh.200 kwa kilo moja atayouza.

“Katika minada ya TANECU (Tandahimba na Newala), MAMCU (Mtwara,Masasi na Nanyumbu), RUNALI (Ruangwa, Nachingwea na Liwale) na ule wa Lindi Mjini wakulima waligoma kuuza korosho zao kwa bei ya Sh. 2,700 kutokana na serikali kuwaahidi kuwa bei ya kilo moja itafikia Sh. 5,000 kwa mwaka huu kwasababu kuna wanunuzi kutoka nchini Marekani.

“Tunaiomba serikali inunue Korosho zote kwa wakulima ili kuwalinda na bei ndogo kutokana na kushuka kwa bei ya korosho kwenye soko la dunia kisha wao wataiuza kwa wanunuzi kwa bei watayoona wao inafaa, “ amesema.

Zitto amesema pia wanapendekeza kasi kwenye ujenzi wa viwanda vya ubanguaji wa korosho ili kuongeza thamani badala ya kuendeleza kusafirisha korosho ghafi kwenda nje ya nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles