31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

ZIMBABWE YAPIGA MARUFUKU UAGIZAJI MAHINDI KUTOKA NJE

HARARE, ZIMBABWE


SERIKALI ya Zimbabwe imepiga marufuku uagizaji wa mahindi kutoka nje, ikiwa ni hatua ya kumlinda mkulima wake dhidi ya ushindani usio wa haki.

Taifa hilo limesema kuwa linatarajia kupata mavuno mengi baada ya kupata mvua ya kutosha.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisa Mkuu wa Masuala ya Uchumi, Prince Kuipa, wakulima wa Zimbabwe wanatarajia kujipatia mavuno ya kutosha kwa chakula na biashara baada ya mvua za kuridhisha kunyesha.

Zimbabwe imekuwa ikipondwa na mitandao ya habari duniani kama inayokaribia kuzama katika utawala mbovu na sera mbaya za kiuchumi.

Lakini kwa sasa inakadiriwa na Benki ya Dunia kuwa katika mkondo wa kupanda kwa uchumi wake kwa asilimia mbili kutoka asilimia sifuri ya mwaka 2016.

Mwaka 2016, taifa hilo lilikumbana na ukame na watu milioni nne walibakia katika baa la njaa.

Kwa miaka 16 sasa, taifa hilo limekuwa likitegemea uagizaji mahindi kutoka nje ya nchi ili kukidhi mahitaji ya chakula, chakula cha mifugo na pia kujiwekea akiba ya taifa.

Hata hivyo, Serikali ya Rais Robert Mugabe (93) ilizindua sera maalumu ya kufufua sekta ya uzalishaji nafaka.

Ni mpango uliogharimu mabilioni ya fedha za taifa hilo, huku wakulima wakiahidiwa bei ya Sh 78,000 kwa kila gunia watakalovuna.

Serikali hiyo ilitoa vifaa muhimu kwa bei nafuu na vingine vikitolewa bure, mpango ambao umeshuhudia manufaa makubwa.

“Kwa sasa tunatarajia mavuno ya tani milioni 3.5 na mikakati yetu ni kujiwekea tani milioni 2.5 katika hazina yetu ya chakula na salio kuelekezwa sekta ya mifugo,” alisema Kuipa.

Uchumi wa taifa hilo, ambalo mwaka jana lilivuna tani 511,000 tu za nafaka, hutegemea kilimo kwa asilimia 70.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles