27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MAREKANI YASEMA HAINA UADUI NA KOREA KASKAZINI

WASHINGTON, MAREKANI


SERIKALI ya Marekani imesema haina mpango wa kutaka mabadiliko ya utawala nchini Korea Kaskazini.

Kali hiyo ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson, imekuja huku hofu ikitanda juu ya mpango wa silaha za nyuklia wa Pyongyang.

“Sisi si maadui zenu,” alisema Tillerson na kuongeza kuwa Marekani ilitaka mazungumzo wakati mmoja.

Pyongyang inadai jaribio lake la hivi karibuni la makombora linaweza kushambulia magharibi mwa Marekani na zaidi.

“Hatutaki mabadiliko ya utawala, hatulengi kuuangusha utawala, hatutaki kuharakisha muungano wa eneo la Peninsula, hatutaki sababu ya kutuma wanajeshi wetu kwenye eneo lenu,” alisema Tillerson, akirejea mpango wa kuziunganisha tena Korea Kaskazini na Korea Kusini.

“Sisi si maadui zenu, sisi si tisho kwenu, lakini mnatuweka katika tisho lisilokubalikana, lazima tujibu,” alisema.

Jaribio la pili la kombora la masafa marefu linaloweza kushambulia bara jingine (ICBM) siku ya Ijumaa, lililosherehekewa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, lilikuwa la karibuni kutekelezwa, linalokiuka marufuku ya Umoja wa Mataifa.

Majaribio hayo ya karibuni yamesababisha hofu kubwa juu ya tishio la Pyongyang dhidi ya Marekani na kuwapo mwito wa haja ya kuzuia shambulio lolote nchini Marekani.

Makao Makuu ya Wizara ya Ulinzi nchini Marekani, Pentagon, yametoa taarifa za hivi karibuni juu ya hatua za kijeshi, lakini wachambuzi wanasema kukabiliana na Korea Kusini itakuwa ni maafa.

Hilo limemfanya Tillerson arudie kwa kirefu kueleza kuwa Marekani hailengi mabadiliko ya utawala na kuongeza kuwa lengo ni kufanya mazungumzo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles