28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

ZIMBABWE YACHUNGUZA PHD YA GRACE MUGABE

HARARE, ZIMBABWE


MAMLAKA ya kukabiliana na ufisadi nchini Zimbabwe imeanza kuchunguza  uhalali wa shahada ya udaktari aliyopewa mke wa Robert Mugabe, Grace.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na  Shirika la Habari Ufaransa (AFP), msemaji wa mamlaka hiyo, Phyllis Chikundura alithibitisha kuanza kwa uchunguzi huo.

 

“Tumethibitisha kuwa kuna ripoti kama hiyo na kwamba kuna uchunguzi kama huo pia,” alisema Chikundura.

 

Grace alidaiwa kupata Shahada hiyo baada ya miezi kadhaa ya masomo mwaka 2014.

 

Shahada hiyo alitunzwa na Mugabe mwenyewe wakati aakiwa rais wa taifa hilo na pia Kansela wa Chuo Kikuu cha Zimbabwe.

Awali wakati akipokea shahada hiyo yenye utata alipongezwa na maafisa wengine wa serikali waliomtetea.

 

Grace alikuwa akitumaini kumrithi mumewe kama kiongozi wa Chama na Taifa, lakini harakati zake zilikwama baada ya jeshi kuingilia kati.

 

Uingiliaji wa jeshi ulisababisha Mugabe kuondoka madarakani baada ya kuwa mtawala wa Zimbabwe kwa kipindi cha miaka 37. Emmerson Mnangagwa ndiye rais wa sasa wa Zimbabwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles