24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

WANAOIKOSOA CCM WASIBEZWE

Na CHRISTINA GAULUHANGA-DAR ES SALAAM


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula, amesema anawapongeza wakosoaji kwakuwa wamekuwa wakichangia kurekebisha mapungufu na kumairisha chama chao.

Akizungumza jana katika hafla fupi ya kumpokea aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Wadhamini na mgombea ubunge wa Ilala kwa tiketi ya Chadema mwaka 2015, Mangula alisema siasa za ukosoaji ni kutoa mawazo na wengine wakarekebisha.

“Kukosoa ni silaha ya mapinduzi, kukiri kosa na kusahihisha ni jambo la msingi, wenzetu wamekuwa ni vyama vya kukosoa CCM, ninawapenda sana na kuwaunga mkono kwani wao wanakosoa kwa kubeza, lakini inatusaidia kujirekebisha,” alisema Mangula.

Alisema CCM ina mipango mikakati ya kukosoa kupitia vikao maalumu vilivyowekwa vya kuangalia katiba na kuirekebisha kwa kuangalia mawazo mapya.

Aliongeza kuwa anamkaribisha mwanachama mpya Hassanali ambaye amezikubali kazi za CCM na kuamua kujiunga nayo.

“Ipo minong’ono pembeni inayosema sisi tumekuwa tukiwanunua wapinzani… fedha hizo hatuna, kwani waumini wanapohama makanisa wanapewa fedha na nani zaidi ya kukubali kinachofanyika upande mwingine?” alihoji Mangula.

Alisema Hassanali ameona fika hawana cha kufanya tena huko walikokuwa kwakuwa hoja zao zote zimefutwa na Serikali ya Rais Dk. John Magufuli.

“Mlilalamikia ufisadi, mikataba mibovu, rasilimali za nchi na mashirika ya umma kutafunwa, lakini chini ya JPM hayo yote yametekelezwa, hamna cha kukosoa sasa,” alisema Mangula.

Hata hivyo, Mangula amewataka wana CCM kuacha kunung’unika na badala yake watumie vikao halali vya chama kujadili mambo yao.

Kwa upande wake, Hassanali alisema kuwa aliitumikia Chadema kwa miaka 15 na amejifunza mambo mengi akiwa ndani ya chama hicho.

Alisema uamuzi wake hajashawishiwa na mtu yeyote  wala kupewa hongo, ila ameweka masilahi ya jamii mbele.

Naye, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole, alimwomba Mangula kuwapa ulinzi wanachama wapya wanaojiunga na chama hicho wakitokea upinzani.

Alisema wanachama hao wamekuwa wakipokea vitisho, kuvunjwa moyo na kutishwa jambo ambalo linahitaji nguvu za wana CCM kuwalinda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles