25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

 BOMBA LA GESI LALIPUKA DAR

Na LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM


MOTO unaodaiwa kusababishwa na kutoboka   bomba la gesi umeteketeza baadhi ya nyumba na vibanda katika eneo la Buguruni kwa Mnyamani,  Dar es Salaam.

Taarifa za   tukio hilo zilianza kuenea katika mitandao ya jamii saa 11:00 na kuzua taharuki kwa wananchi.

Iilielezwa kuwa  nyumba zaidi ya tatu ziliwaka moto katika eneo la Buguruni kwa Mnyamani  kutokana na moto huo wa bomba la kusafirisha gesi lililopasuliwa.

Mashuhuda waliiambia MTANZANIA kuwa mafundi wa Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam( Dawasco) walikuwa wanabadilisha mabomba ya maji ndipo walipolipasua bomba hilo la gesi linalopita katika eneo hilo.

Kupasuka kwa bomba hilo kulisababisha watu kukimbia huku na kule ili kuuona huku wengine ikiwa ni njia ya kujinusuru.

Hali hiyo ilisababisha barabara ya Buguruni kwa Mnyamani kwenda Vingunguti kufungwa huku treni inayofanya safari kati ya Stesheni na Ubungo ikisimamisha safari kutokana na moto huo.

Akizungumzia hali hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kapuulya Msomba alisema  bomba hilo lilipasuliwa na wafanyakazi wa Dawasco.

“Tunashuru zimamoto wameshafika hapa hivyo hakuna tabu, tunaimani watauzima moto huo.

“Ninachowaomba wananchi wasikimbilie eneo lenye hatari, wawaachie Kikosi cha Zimamoto wafanye kazi yao,’’ alisema Msomba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles